HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 10, 2021

BANK OF AFRICA YASHEREHEKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Dar Es Salaam:

Huduma kwa Wateja inabaki kuwa sehemu muhimu ya BANK OF AFRICA. Uvumbuzi, utowaji na upokeaji wa huduma kwa wateja ni kitovu cha huduma bora. Tunaendelea kuahidi huduma bora kwa wateja kama inavyoelezwa katika hati yetu ya huduma (Service charter) ambayo inajumuisha haki, usiri, uaminifu na uwazi kwa mteja, maadili ambayo yamejumuishwa kwa wafanyikazi wa benki yetu.

Akizungumza wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Mkurugenzi Mtendaji wa BANK OF AFRICA, Bwana Adam Mihayo alisema, "Huduma kwa Wateja inabaki kuwa eneo kuu la kuzingatia katika shughuli zetu za kila siku kama Benki. Tunasherekea wiki hii ya huduma kwa wateja mwaka huu na kaulimbiu ya "Nguvu ya Huduma (the power of Service)." Katika hili Benki imeanza maboresho mashuhuri na ya msingi ya utoaji wa huduma ambayo yatapelekea huduma zetu kupatikana katika nyanja mbali mbali ili kuweza kumfikia na kumsaidia mtanzania.

Hivi sasa, wateja wetu wanafurahia huduma zetu zinazopatikana katika njia mbali mbali, na kupelekea kuridhika kwa wateja huku wengi wao wakirudi na kutoa ushuhuda mzuri wa jinsi walivyo patiwa huduma bora pale watumiapo matawi yetu au huduma kupitia njia mbadala. Mkurugenzi Mtendaji anaendelea kuwahakikishia wateja maendeleo zaidi na mazuri ya kiteknolojia ambayo yatasanua upeo mpya na namna bora ya utowaji huduma. Mabadiliko haya yataunda njia na vile vile kupanua upatikanaji wa huduma kwa urahisi kwa kujumuisha mifumo mbali mbali ya kidigitali, kama vile, huduma kwa njia ya simu ya Mkononi, huduma kwa njia ya Mtandao, na huduma za Kadi mbali mbali. Benki pia ilipanua safu ya malipo na ukusanyaji wa fedha kwa kuanzisha mifumo ya BOA Pay ambayo huwawezesha wateja kufanya malipo na makusanyo wakiwa katika maeneo yao ya kazi au wakiwa nyumbani.

Tunaamini utowaji wa huduma bora utaendelea kuangazia na kuongeza uridhikaji wa wateja wetu na ukuaji wa biashara zao, ambao utapelekea ukuwaji sambamba wa shirika letu. Leo, benki imeandaa huduma maalum kwa wateja wake, kuwakumbusha na kujikumbusha sisi wenyewe kama wafanyikazi, umuhimu na thamani ya wateja wetu”.

Mapema mwaka huu BANK OF AFRICA iliwekwa kuwa miongoni mwa benki 15 zinazoongoza barani Afrika, ikiwa na mtaji wa dola bilioni 2.5, tunaamini hatua hii kubwa isingeweza kutimizwa bila wateja wetu wapendwa. Hivyo basi, benki inaahidi kuendelea kuhudumia wateja kwa bidii, hii ikiwa kipaumbele cha msingi katika Biashara yetu. Ukuaji huu unatokana na maboresho ya shughuli za benki, uwepo wa mikakati iliyobora na njia bora za huduma kwa wateja, BANK OF AFRICA imejitolea kutoa elimu ya kifedha kwa wateja wa mahitaji mbali mbali, ikilenga hasa wafanya biashara wadogo na wakati (SMEs) ili kupanua ujuzi juu ya usimamizi wa fedha na maendeleo yao. Benki imewezesha matawi yake na wafanyakazi waliobobea katika kujenga mahusuani bora ambao wanapatikana katika matawi yetu yote 20 nchini kote.

BANK OF AFRICA-TANZANIA inajivunia kuwa moja katika ya benki ndani ya Group BANK OF AFRICA katika utekelezaji wa shughuli zake zote. Benki inaelekea kuongeza nguvu kwa kutumia mtandao wa BMCE BANK OF AFRICA kwa kutoa huduma kwa wateji wanao agiza na kutoa mizigo ndani na nje ya Tanzania. Group BANK OF AFRICA imejikita katika dhamira na maono yake ya kuhakikisha maendeleo ya wadau wake, kuendesha ukuaji wa uchumi mahali benki ilipo, kuboresha huduma kwa wateja na kuwa benki inayopendelewa katika masoko yake, BANK OF AFRICA inajumuhisha mchanganyiko mbali mbali wa mbinu za utendaji ambazo zimethibitisha ufanisi katika nchi 18.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad