HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 7, 2021

AKAMATWA NA SILAHA AINA YA RIFLE INAYODHANIWA KUTUMIKA KWENYE UJANGILI-ACP MALULU

 Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

JESHI la polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, linamshikilia mtuhumiwa mmoja jina linahifadhiwa, kwa kukutwa na silaha aina ya Rifle yenye no.373 inayodhaniwa kutumika kwenye matukio ya ujangili.

Kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Rufiji ACP Kungu Malulu alithibitisha ,kukamatwa kwa mtu huyo, huko katika Kijiji cha Mwangaei Kibata kata ya Kitamba tarafa ya Kipatimu wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi wakati askari polisi mkoa wa Kipolisi Rufiji kwa kushirikiana na kikosi cha kuzuia na kupambana na ujangili nchini wakiwa katika msako.

"Walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja mwanaume mwenye umri wa miaka 43,mkulima mkazi wa Mwangei akiwa na silaha aina ya Rifle yenye no 373 ambayo alikuwa akimiliki kinyume cha sheria na kutumia katika ujangili."

Katika hatua nyingine Kamanda Malulu alisema ,walimkamata mtuhumiwa mmoja mwanaume akiwa na silaha aina ya Gobore alilokuwa kaliticha juu ya dali la nyumba yake ,katika kijiji Kitembo wilayani Kibiti .

Hata hivyo wamewakamata watuhumiwa wengine wawili wakazi wa Dar es Salaam wanaume, wakisafirisha viroba vitano vinavyodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya aina ya bangi yenye uzito wa kg 130.

"Watuhumiwa hawa walikuwa wakitumia gari aina ya T 559BJL Toyota Corona watuhumiwa wote wanahojiwa kwa upelelezi na watafikishwa mahakamani."

Kungu Malulu alisema watuhumiwa wote majina yanahifadhiwa kutokana na sababu za kiupelelezi.

Kufuatia matukio hayo, Malulu alitoa wito kwa wananchi, kuzingatia taratibu za kumiliki silaha bila kutumia pasipo uhalali na wale wanaomiliki kihalali wahakikishe wanazingatia matumizi sahihi ya silaha zao.


Kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Rufiji ACP Kungu Malulu akizungumza na waandishi wa habari wakati walipomkamato mtu mmoja aliyekuwa na siraha pasipo kuwa na kibali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad