Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akizungumza na wananchi wa kata ya Mgama akiongelea maswala ya ramri chonganishi ambazo zinachochea migogoro kwa wananchi wa kata hiyo
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Bashir Muhoja akizungumza na wananchi wa kata ya Mgama akiongelea maswala ya ramri chonganishi ambazo zinachochea migogoro kwa wananchi wa kata hiyo
Baadhi ya wananchi wakiwasikiliza viongozi kutoka wilaya ya Iringa walipofika kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchiNa Fredy Mgunda,Iringa.
Baadhi yawananchi katika Kijiji Chai
Itwaga wilayani Iringa wameilalamikia Serikali kwa kushindwa kuwadhibiti
waganga wa asili wanaopiga ramri chonganishi na kuibua uhasama unaohatarisha
amani katika jamii.
Wakizungumza katika Mkutano wa hadhara
baadhi ya Wananchi hao walisema hali ya usalama katika Kijiji hicho imekuwa
ndogo kutokana na waganga kuwaaminisha wananchi juu ya Ushirikiana uliokithiri
huku Serikali ikiendela kukaa kimya pasipo kuwakemea.
Walisema kuwa kumekuwa kukitokea kwa
matukio mengi kijijini hapo na yote yamekuwa yakihusiswa na imani za
kishirikina jambo linalochangia kuwaita waganga wa kienyeji kutoka nje ya
kijiji hicho kwenda kufanya ramri chonganishi kwa wananchi.
Wananchi hao walisema kuwa hivi
karibuni kulitokea ajali ya pikipiki kugongana na kusababisha vifo kwa wananchi
wa kijiji hicho jambo ambalo nalo lilichukuliwa kama ajali iliyotokana na
maswala ya ushirikina.
Walisema kuwa waganga hao wa jadi
ambao wamekuwa wakifika kijijini hapo na kupiga ramri chonganishi wamekuwa
wakifanya kazi bila ya kuwa na kibali maalum kutoka serikali na kujifanyia mambo
wanayokata kwa kuchochoe uhasama kwa wananchi.
“Hivi tunaomba kuuliza kuwa kweli
serikali ya kijiji ipo au maana waganga hawa wa kienyeji wamekuwa wanaingia
kijijini hapa na kufanya shughuli ya kupiga ramri chonganishi na serikali
imekuwa haiwachukulii hatua yoyote ile eti viongozi kutoka wilayani unalikubali
hilo?” walisema wananchi.
Awali akitoa taarifa kwa niaba ya
mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Iringa Joel Msiba ambaye ni mpelelezi wa
tarafa ya Kiponzero na .....alisema kuwa kijijini hapo kumekuwa na imari za
kishirikiana kwa kuwaita waganga wa kienyeji kuwanywesha dawa za kienyeji
ambazo zimekuwa zikichochea ugomvi baina ya wananchi na wananchi.
Alisema kuwa hivi karibu kulitokea
ajali ya pikipiki katika kijiji hicho na kupelekea wanananchi kuwaleta waganga
wa kienyeji kupiga ramri chonganishi ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo
kwa wananchi .
Afande msiba alisema kuwa wananchi wamekuwa wakitoa
kiasi cha pesa zaidi ya shilingi laki saba kwa ajili ya kulipia ramri kwa
waganga jambo ambalo limekuwa likichangia uchonganishi kwa jamii inayoishi
katika kijiji hicho.
Alimalizia kwa kuwataka wananchi wa
kijiji cha Itwaga kuacha mara moja tabia hiyo ambayo imekuwa ikiwachonganisha
wananchi lakini imekuwa ikididmiza uchumi wa wananchi kwa kutoa kiasi kikubwa
cha pesa kwa ajili ya waganga badala ya pesa hiyo kufanyia shughuli nyingine za
kimaendeleo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Iringa Bashir Muhoja alisema kuwa ni kosa kubwa kwa
mtendaji wa kata,kijiji kumruhusu mganga wa kienyeji kufanya kazi yoyote kwenye
kijiji au kata bila ya kuwa na kibali maalum kutoka kwa viongozi husika.
Alisema kuwa waganga wa kienyeji
hawarusiwi kufanya kazi yeyote ile kijijini bila kuwa na kibali hivyo ikitokea
mtendaji yoyote yule ameruhusi jambo hilo bila kibali maalum basi mtendaji huyo
atachukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria kwa mujibu wa mkataba wake wa
ajira serikalini.
Naye mkuu wa wilaya ya Iringa
Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa swala la ramri chonganishi haliruhusiwi kwa
kuwa limekuwa linahatarisha usalama wa wananchi kwa kuwa hata serikali
hailikubari swala hilo.
Alisema kuwa ni marufuku kupiga
ramri chonganishi katika vijiji au kata hivyo watendaji wote marufuku kutoa
kibali chochote kile kwa ajili ya kufanya ramri chonganishi kwa kuwa swala hilo
limekuwa likichochea migogoro kwa wananchi.
Moyo alisema kuwa ni marufukuwa kwa
watendaji wote wa wilaya ya Iringa kutoa vibari kwa ajili ya ramri chonganishi
katika wilaya hiyo kwa lengo la kuondoa migogoro ya wananchi inayotokana na
hizo ramri changanishi.
No comments:
Post a Comment