HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 17, 2021

UJUMBE WA TPSF KUKUTANA NA WAWEKEZAJI MAREKANI

 

UJUMBE wa Wafanyabiashara kutoka Sekta Binafsi ukiongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bi. Angelina Ngalula Septemba 16,2021 umeondoka kuelekea nchini Marekani kwa ziara ya Kibiashara ambayo imeandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi kwa kushirikiana na taasisi ya Marekani Corporate Council on Africa.

Taarifa ya kwa umma iliyoandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano-TPSF imeeleza kuwa Ujumbe wa Sekta Binafsi utakutana na wawekezaji wakubwa katika sekta mbalimbali zikiwemo sekta za afya, utalii, miundombinu, kilimo na teknolojia ya Habari.

Hata hivyo taarifa hiyo imeeleza kuwa Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za sekta binafsi za kuunga mkono juhudi kubwa za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania za kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia wawekezaji wa nje na ndani, pamoja na kazi kubwa anayoifanya ya Re-Branding Tanzania.

"Ziara hii ni matokeo ya mkutano ambao Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi alifanya na Mhe. Donald Wright, Balozi wa Marekani nchini Tanzania, ambapo Bi. Ngalula, alimwomba Mh. Balozi kusaidia sekta binafsi ya Tanzania kwa kuwaunganisha na wawekezaji wakubwa wa Marekani ili waweze kuungana na wafanyabiashara wa Tanzania katika utekelezaji wa miradi ya ubia (Public Private Partnership) na kuwekeza katika sekta za utalii, uvuvi, afya, miundombinu, ujenzi wa Industrial Parks na kukuza biashara na masoko kupitia mpango wa AGOA." Imeeleza taarifa hiyo

Licha ya hayo Taasisi ya Sekta Binafsi inaishukuru serikali kupitia Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ubalozi wa Tanzania New York na Washington Marekani na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzani kwa ushirikiano mkubwa uliowezesha ziara hii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad