HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 14, 2021

RC TABORA AWATAKA WAHITIMU WA JKT OPERESHENI SAMIA SULUHU KUENDELEZA UZALENDO WATAKAPOKUWA VYUONI

 

 NA TIGANYA VINCENT

WAHITIMU  wa Mafunzo ya Awali ya Kijeshi wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria chini ya operesheni Samia Suluhu wametakiwa kuwa mfano wa uzalendo na kuigwa watakapojiunga na vyuo mbalimbali hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani wakati akifunga mafunzo ya awali ya Kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria chini ya operesheni Samia Suluhu.

Alisema wawapo Vyuoni wanatakiwa kuwa mabalozi kwa kuonyesha na kuendeleza uzalendo waliofundishwa Msange JKT ili wawe tofauti na Vijana ambao hawakubahatika kupata mafunzo.

Mkuu wa Tawi la Mafunzo na Operesheni kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Aisha Matanza alisema wahitimu hao wanatakiwa kuwa macho na masikio ya Watanzania dhidi ya maadui wa ndani na nje wa Tanzania.

Alisema wantakiwa kutumia mafunzo hayo kwa ajili ya maslahi ya Nchi na Watanzania na kuwa tayari kuitumikia nchi katika maeneo mbalimbali kwa uzalendo.

Kamanda wa Kikosi cha Msange JKT Kanali Sadick Mihayo alisema wahitimu hao walianza mafunzo Mwezi Juni mwaka huu wakiwa 1,533 lakini walifanikiwa kuhitimu ni 1,503.

Alisema katika cha mafunzo wahitimu hao wamefundishwa kozi za awali za kijeshi, shughuli za ujenzi , ujasiriamali kama vile utengezaji wa sabuni , ufugaji wa nyuki , michezo , maandalizi ya mashamba na shughuli za utamaduni.

Kanali Mihayo alisema mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali za kujitegemea.

Akisoma risala kwa niaba ya wenzake Caroline Tibamanya aliiomba Serikali kuongeza muda wa mafunzo kwa Mujibu wa Sheria ili wahitimu wengi waweze kunufaika na elimu inayotolewa na JKT.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( wa pili kutoka kushoto) akipokea salamu leo kutoka kwa Maafisa wa Jeshi kwenda kufunga  mafunzo ya awali ya Kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria yanayojulikana  kama operesheni Samia Suluhu.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( wa pili kutoka kulia) akishirikiana na Maafisa wa Jeshi na Wahitimu wa mafunzo ya awali ya Kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria yanayojulikana kama  operesheni Samia Suluhu kuimba wimbo wa kuhamasisha uzalendo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( katikati waliokaa ) akiwa katika picha ya pamoja na  Maafisa wa Jeshi baada ya kufunga leo mafunzo ya awali ya Kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Msange JKT kwa mujibu wa Sheria ambayo yaliyopewa jina la Oporesheni Samia Suluhu. Picha na Tiganya Vincent


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad