Njombe wazidi kupambana na kiwango cha udumavu kwa kuhamasisha ulaji mlo kamili - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 17, 2021

Njombe wazidi kupambana na kiwango cha udumavu kwa kuhamasisha ulaji mlo kamili

 Na Amiri Kilagalila, Njombe

Serikali mkoani Njombe inaendelea kutoa elimu kwa wananchi wa mkoa huo ili kupunguza kiwango cha udumavu ambao kwa sasa kiwango chake cha udumavu ni asilimia 53.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Njombe Injinia Marwa Rubirya wakati akizungumza ofisini kwake kwa mabolozi nane kutoka umoja wa ulaya ambapo wamefika mkoani hapo na kutembelea utekelezaji wa mradi wa AGRI - CONNECT unaotekelezwa mkoani Njombe kwa wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha mbogamboga na matunda na kubainisha kuwa ujio wa mradi huo umesaidia kuelimisha zaidi jamii kuhusui umuhimu wa kuzingatia mlo kamili.

“Usitegemee maofisa wa mradi watakuja wachukue mboga wakuwekee mdomoni ndio maana nasema hata sisi tuna wajibu wa kubadirika na kuona kuwa hivi vyote vinavyoletwa vinasaidia kutubadilisha sisi na maisha ya watoto wetu,kuzalisha ni kitu kimoja na kuvitumia ni jambo jingine”alisema Rubirya

Aidha mkuu wa mkoa wa Njombe amewataka wananchi mkoani hapo kubadiri mfumo wa maisha ili kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau mbalimbali kukomesha udumavu huku akizialika nchi za umoja wa ulaya kuja nchini kuwekeza katika mazao ya Mbogamboga na Matunda.

“Lakini bado tuna shida kubwa ya udumavu na utapiamlo kwa watoto wetu na mimi nitoe wito vyakula hivi tulivyonavyo tuvitumie kuhakikisha watoto wetu wanapata mlo kamili.Na mkoa wa Njombe tunasema zipo fursa nyingi sana za uwekezaji katika mkoa wetu”alisema Rubirya

Baadhi ya wakulima wa Mbogamboga na matunda mkoani Njombe akiwemo Huruma Mgaya wameshukuru shirika la AGRI-CONNECT kwa kuwapa elimu ya kuzalisha mbogamboga na matunda ambapo wamesema tangu wameanza hivi sasa wanaona mabadirikiko makubwa katika maisha yao.

“Awali bustani za nyumbani tulikuwa tunatumia vitalu vikubwa na maji mengi kumwagilia lakini shirika lilivyokuja kutufundisha tunamwagila lita moja tunapata mboga na nyumbani kwangu siwezi kukosa mboga”amesema Huruma Mgaya

Ronadi Mtana ni mtaalamu kutoka mradi wa AGRI-CONNECT unaotekelezwa katika mikoa ya Njombe na Iringa ameeleza dhima ya ujio wa mabalozi kutoka umoja wa ulaya.

“Lengo hasa ni kuweza kuona mradi huu mkubwa ambao wameuwezesha kwa serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa URO milioni 100 na URO milioni 50 zimekwenda kwenye ujenzi wa barabara na hizi zingine zimekwenda kwa wakulima kupitia taasisi zisizokuwa za kiserikali takribani saba,kwa hiyo wamekuja kuona shughuli zinazofanyika”amesema Ronati Mtana

Moja ya kitalu kidogo cha mbogamboga kilichotembelewa na wageni hao
Wageni walipofika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Njombe kabla ya kuwatembelea wakulima wadogo mkoani humo.
Baadhi ya wageni kutoka umoja wa ulaya waliofika mkoani Njombe wakishangilia jambo katika maonyesho waliyoyapata kwa mmoja wa mkulima mdogo mkoani Njombe.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya akizungumza mara baada ya kupokea ugeni huo ofisini kwake wenye lengo la kuona matumizi ya fedha zilioletwa kwa ajili ya matumizi mbali mbali.


B:


C:


D:.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad