HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 2, 2021

MEJIMENTI MPYA YAANZA KAZI MAKAO MAKUU YA PAPU

 

Waziri wa TEHAMA na Huduma za Posta nchini Zimbabwe Mhe. Supa Mandiwanzira akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) jijini Arusha, Tanzania kushuhudia makabidhiano ya ofisi ya Katibu Mtendaji Mkuu wa umoja huo ; anaeshuhudia ni Katibu Mkuu Mtendaji wa umoja huo aliemaliza muda wake Ndugu Younouss Djibrine. PICHA NA: TCRA

Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika, (PAPU) anayemaliza muda wake Ndugu Younouss Djibrine ( kushoto) akikabidhi Ofisi kwa Katibu Mkuu Mtendaji Mpya Ndugu Sifundo Chief Moyo kwenye Ofisi za PAPU Jijini Arusha, leo Tarehe 1 Septemba 2021. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kutoka kulia), Waziri wa TEHAMA na Huduma za Posta Zimbabwe na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania( TCRA) Dkt. Emmanuel Manasseh (wa kwanza kushoto). PICHA NA: TCRA
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt Faustine Ndugulile (Mb) akitoa hotuba kwa washiriki wa Mkutano wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) uliofanyika jijini Arusha mapema juma hili. Washiriki wa Mkutano huo wameshuhudia makabidhiano ya ofisi baina ya Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja huo aliemaliza muda wake Younouss Djibrine Katibu Mkuu Mtendaji mpya Ndugu Sifundo Chief Moyo. PICHA NA: TCRA
Kutoka kulia ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Tanzania Mhe. Dkt Faustine Ndugulile (Mb) akiwa sambamba na Waziri wa TEHAMA na Huduma za Posta nchini Zimbabwe Mhe. Supa Mandiwanzira wakifuatilia shughuli za mkutano wa makabidhiano ya Ofisi ya Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) jijini Arusha mapema wiki hii. Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa umoja huo Ndugu Younouss Djibrine (Cameron) amekabidhi ofisi kwa Ndugu Sifundo Chief Moyo(Zimbabwe). PICHA NA: TCRA
Washiriki wa Mkutano wa Makabidhiano ya ofisi ya Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) wakiongozwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Tanzania Mhe. Dkt Faustine Ndugulile. Katika Mkutano huo uliofanyika makao makuu ya PAPU jijini Arusha, Tanzania; Ndugu Younouss Djibrine (Cameron) (wa pili mstari wa pili kulia) amekabidhi ofisi kwa Ndugu Sifundo Chief Moyo(Zimbabwe) wa kwanza mstari wa pili kulia). PICHA NA: TCRA

*MAKABIDHIANO YA OFISI KATI YA MENEJIMENTI ILIYOMALIZA MUHULA WAKE UMOJA WA POSTA AFRIKA (PAPU), ARUSHA, TANZANIA.

MEJIMENTI mpya ya chombo cha sekta ya posta barani Afrika, Umoja wa Posta Afrika (PAPU) imeanza kazi leo, tarehe 1 Septemba 2021 kufuatia sherehe iliyofana iliyofanyika kwenye jengo la uwekezai PAPU, makao makuu Arusha mjini mkoani Arusha.

Katibu Mkuu WA PAPU aliyemaliza muhula wake, Bwana Younouss Djibrine; alikabidhi uongozi kwa Katibu Mkuu mpya wa Umoja huo, Bwana Sifundo Chief Moyo kwenye shughuli ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Dr. Faustin Ndugulile (Mb.).

Kma sehemu ya mabadiliko ya uongozi katika chombo hicho cha bara la Afrika, Katibu Mkuu Msaidizi aliyemaliza muhula wake kwenye Umoja huo, Bwana Kolawole Aduloju pia alikabidhi ofisi kwa Bi. Jessica Hope Uwera Sengooba.

PAPU inaendele kutekeleza majumumu yake muhimu ya kujenga ENEO MOJA LA SHUGHULI ZA POSTA wakati wote na katika mazingira yote, kama mchango wake kwenye kufikia azma ya pamoja na ya muda mrefu ya watu wa Afrika ya kuleta maendeleo shirikishi na endelevu kwa jamii.

Mabadiliko ya menejimenti ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) yameainishwa kwenye utaratibu rasmi wa kukabidhiana madaraka kwa mpangilio baada ya kumalizika kwa muhula wa uongozi wenye mafanikio makubwa.

Menejimenti mpya inaingia ofisini kipindi cha janga la UVIKO-19 ambalo limevuruga shughuli za mifumo ya shughuli za kibiashara na ambalo linahofiwa kuleta athari za muda mrefu kwenye maendeleo ya kawaida ya biashara na kwa hivyo kuibua changamoto kwa umma kwa ujumla kutathmini upya njia bora za kukabili athari hizo.

Mikakati ya kutathmini upya na kukabili hali hii inahitajika ili kuweza kugeuza changamoto zilizojitoketa kuwa fursa kwa ama kubadilimifumo ya utoaji huduma au kubadili bidhaa na huduma zinazotolewa ili kuendelea kuwa na wateja na hivyo kuendeleza biashara. Hii itachangia katika kulinda sekta ya posta na kuimarisha uwezo wake wa kugundua mapema na kukabiliana na majanga mengine kama haya mbeleni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad