HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 15, 2021

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AWATOA WITO KWA SHIRIKISHO LA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman, ametoa wito kwa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar, kuhamasisha na kuelemisha wananchi kuendeleza maridhiano ya Serikali ya Umoja wa kitaifa ambayo ni muhimu katika kusaidia kujenga amani ya nchi.

Mhe. Othman  ameyasema hayo leo  ofisini kwake Migombani alipozungumza na Uongozi wa Shirikisho la Jumuiya za Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA).

Amefahamisha kwamba hatua hiyo ni muhimu kwa kutasaidia katika kujenga amani ya kweli kwani bila ya kuwepo kunaweza kuchangia kuongezeka idadi ya watu wenye Walemavu .

Amesema ni muhimu ajenda ya kuhubiri suala hilo ikabebwa na kila mmoja ama taasisi miongoni mwa wanajamii  na kila mmoja kujiona na muhusika wa kuhubiri serikali ya umoja wa kitaifa.

Aidha Mhe. Othman ametaka jamii kuachana na utamaduni wa kufanya mambo na matendo yanayoweza kusababisha ajali na kuongeza idadi ya walemavu.

“ Utakuta mtu anaendesha gari, ama baiskeli huku ana anasikiliza simu kwa kuwa anataka kumridhisha mtu mwengine na kusahau kwamba jambo hilo ni hatari na linaweza kusababisha ulemavu na kuongeza idadi ya watu wenye ulemavu” , alitanabahisha Mhe. Makamu wa Rais.

Aidha Mhe. Othman amewaeleza wanajumuiya hiyo kwamba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na watu wenye ulemavu katika kusaidia kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Zanzibar Nd. Ali Omar Makame ame seshauri serikali kufanya utafiti makhususi ili kuibua na kufahamu sababu za kuongezeka tatizo la ulemavu Zanzibar.

Alisema kwamba kwamba pia kunahaja ya  kuwepo jimbo la watu wenye ulemavu ili kupata uwakilishi sahihi zaidi wa watu wenye ulemavu katika vyombo  vya kutunga sheria badala ya utaratiubu  wa sasa kupitia kwenye vyama vya siasa.

Wakati huo huo , Mhe. Makamu wa Rais amekutana na kuzungumza na ujumbe wa  Taasisi inayosaidia vijana kupata fursa za masomo nje ya nchi ya CARI VISION na kueleza kwamba  vijana hao wanafanya jambo jema, lakini pia ni muhimu kuangalia mazingira ya vijana katika vyuo na taasisi wanazokwenda kusoma nje ya nchi.

Mhe. Makamu aliwataka Taasisi hiyo kuandaa mfumo bora zaidi utakaowezesha kuwasaidia vijana  kupata elimu bora inayolingana na mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

“ wakati mwengine mazazi anataka kujiridhisha kujua namna na hali ya elimu inayotolewa , mazingira ya kijana anavyoishi na mambo mengine ni vyema pia na hili likawa miongoni mwa mambo manayoyafanyia kazi” alitanabahisha Mhe. Makamu.

Naye Meneja wa Taasisi hiyo ya CARI VISION yenye makao yake Makuu Mjini Dar es Salaam Yusuph Mohammed ameomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kuwapa ushirikiano zaidi ili kuwasaidia vijana kupata elimu nje ya nchi kwa ngazi na kada mbali mbali.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman ( Katikati) akizungumza na viongozi wa  Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar jana ofisini kwake Migombani . kushoto ni Makamu  Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo  nd. Ali Omar Makame . Picha kwa hisani ya ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman ( Katikati) akizungumza na viongozi wa  Taasisi inayosaidia Vijana kupata fursa za masomo nje ya nchi jana ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar . kushoto ni Nd. Yussuph Mohamed Selemani ofisa wa Taasisi hiyo hapa Zanzibar na Bi SirA Ubwa Mamboya ambaye ni Mlezi wa Taasisi hiyo . Picha kwa hisani ya ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman ( Katikati) akizungumza na viongozi wa  Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar jana ofisini kwake Migombani . kushoto ni ni Makamu  Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo  nd. Ali Omar Makame na  Nd. Bakari Omar Hamar mratibu wa wa miradi wa Jumuiya hiyo. Picha kwa hisani ya ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad