Kamishina
wa Ushirikishwaji wa Jamii, Dkt Mussa Ali Mussa akishirikiana na
vikundi vya sungusungu vya Buhulyo, Isagenhe na Zugimlole kucheza na
kuimba nyimbo za kabila za kisukuma jana katika Kata ya Isagenhe Tarafa
ya Bukene Wilaya ya Nzega Mkoa wa Tabora ikiwa ni siku ya pili ya ziara
yake ya ukaguzi wa uwepo wa Polisi Kata akishirikiana pia na taasisi ya
Hans Seidel Foundation kutoa elimu kuhusu mpango wa Polisi Kata kama
nynzo muhimu itakayosaidia kushughulika na kero za wananchi kuanzia
ngazi ya Kata. Kamishna Dkt. Mussa na Taasisi ya Hans Seidel Foundation
wametoa elimu hiyo kwa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa na Wilaya,
Watendaji wa Kata na Vijiji pamoja, Kamati za Maendeleo za Mkoa na
Wilaya pamoja na wananchi.
Kamishina wa Ushirikishwaji wa Jamii, Dkt Mussa Ali Mussa akizungumza na
wananchi wa Kata ya Isagenhe Tarafa ya Bukene Wilaya ya Nzega ikiwa ni
siku ya pili ya ziara yake ya ukaguzi wa uwepo wa Polisi Kata na kutoa
elimu kuhusu Mpango wa Polisi Kata. Meneja Miradi wa Shirika la Hans Seidel Foundation (HSF) Kadele Mabumba
akizungumza na wananchi wa ya Isagenhe Tarafa ya Bukene Wilaya ya Nzega
Mkoa wa Tabora walipokua katika ziara ya Pamoja na Kamishna wa
ushirikishwaji wa Jamii ya kutoa elimu kuhusu Mpango wa Polisi.
Kamishina wa Ushirikishwaji wa Jamii, Dkt Mussa Ali Mussa akimkabidhi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Safia
Jongo vitabu vya Mpango wa Polisi Kata Tanzania kwa ajili ya kuwakabidhi
watendaji wa Kata wa Wilaya ya Nzega ili vitabu hivyo viwasaidie katika
utekelezaji wa Mpango wa Polisi Kata. Askari wa Sungusungu vikundi vya Buhulyo, Isagenhe na Zugimlole wa Jamii
ya kisukuma wa Kata ya Isagenhe Tarafa ya Bukene Wilaya ya Nzega
wakiimba na kucheza jana wakati wa ziara ya Kamishina wa Ushirikishwaji
wa Jamii, Dkt Mussa Ali Mussa alipowatembelea katika Kata hiyo ikiwa ni
siku ya pili ya ziara yake ya ukaguzi wa uwepo wa Polisi Kata na kutoa
elimu kuhusu Mpango wa Polisi Kata.
No comments:
Post a Comment