HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 27, 2021

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KILIVYOZINDUA KAMPENI ZAKE JIMBO LA USHETU MKOANI SHINYANGA

 

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM ( Bara) Ndugu Christina Mndeme akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Ushetu kwa tiketi ya CCM  Ndugu Emmanuel Cherehani (kulia) kwenye viwanja vya Nyamilangano.Chama Cha Mapinduzi kimezindua rasmi kampeni zake katika jimbo la Ushetu tarehe 26 Septemba 2021.(Picha na Adam Mzee/ CCM Makao Makuu


Naibu Katibu Mkuu wa CCM ( Bara) Ndugu Christina Mndeme akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 mgombea wa ubunge jimbo la Ushetu kwa tiketi ya CCM  Ndugu Emmanuel Cherehani (kulia) kwenye viwanja vya Nyamilangano. Chama Cha Mapinduzi kimezindua rasmi kampeni zake katika jimbo la Ushetu terehe 26 Septemba 2021.(Picha na Adam Mzee/ CCM Makao Makuu)
 

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi  (Bara) Ndugu Christina Mndeme, leo amezindua kampeni za ubunge jimbo la Ushetu wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga.

Mndeme, amesema mgombea huyo Emanuel Peter Cherehani, anatosha kurithi viatu vya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo ambaye pia alikuwa Waziri wa Ulinzi, marehemu Elias Kwandikwa.

Uzinduzi wa kampeni hizo umefanyika katika viwanja vya Nyamilangano, ambapo CCM kimetumia fursa hiyo kumsimamisha Ndugu Emmanuel Peter Cherehani na kumkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya 2020/2025 ya Chama hicho.

Katika hatua hiyo, Mndeme alisisitiza kuwa Chererehani ana uzoefu wa uongozi katika kutetea maslahi ya wananchi wa Ushetu, hususani katika masuala ya kilimo, elimu, afya na maboresho ya miundombinu.

Aliongeza kuwa, mgombea huyo amekuwa Mwenyekiti wa vyama mbalimbali vya ushirika ikiwemo cha wakulima wa Tumbaku,Chama cha Mwadui na Ubangwa na mtetezi wa maendeleo ya wakulima wa pamba.

Katika mkutano huo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali walihudhuria akiwemo Katibu wa Oganaizesheni  wa CCM Ndugu Maudline Castiko, wabunge wa mkoa wa Shinyanga na mamia ya wananchi.

Sehemu ya Watu waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za CCM katika jimbo la Ushetu kwenye viwanja vya Nyamilangano. (Picha na CCM Makao Makuu)
Sehemu ya Watu waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za CCM katika jimbo la Ushetu kwenye viwanja vya Nyamilangano. (Picha na CCM Makao Makuu)
Naibu Katibu Mkuu wa CCM ( Bara) Ndugu Christina Mndeme akiteta jambo na mgombea wa ubunge jimbo la Ushetu kwa tiketi ya CCM  Ndugu Emmanuel Cherehani (kulia) kwenye viwanja vya Nyamilangano.Chama Cha Mapinduzi kimezindua rasmi kampeni zake katika jimbo la Ushetu terehe 26 Septemba 2021.(Picha na Adam Mzee/ CCM Makao Makuu)
Naibu Katibu Mkuu wa CCM ( Bara) Ndugu Christina Mndeme  na mgombea wa ubunge jimbo la Ushetu kwa tiketi ya CCM  Ndugu Emmanuel Cherehani (kulia) kwenye viwanja vya Nyamilangano wakiwapungia mkono wananchi waliojitokeza kwenye ufunguzi wa kampeni.Chama Cha Mapinduzi kimezindua rasmi kampeni zake katika jimbo la Ushetu terehe 26 Septemba 2021.(Picha na Adam Mzee/ CCM Makao Makuu)
Naibu Katibu Mkuu wa CCM ( Bara) Ndugu Christina Mndeme akihutubia wananchi wa Ushetu ikiwa siku ya kwanza ya uzinduzi wa kampeni kwenye viwanja vya Nyamilangano.Chama Cha Mapinduzi kimezindua rasmi kampeni zake katika jimbo la Ushetu terehe 26 Septemba 2021.(Picha na Adam Mzee/ CCM Makao Makuu)

Mgombea wa ubunge jimbo la Ushetu kwa tiketi ya CCM  Ndugu Emmanuel Cherehani kwenye viwanja vya Nyamilangano.Chama Cha Mapinduzi kimezindua rasmi kampeni zake katika jimbo la Ushetu terehe 26 Septemba 2021.(Picha na Adam Mzee/ CCM Makao Makuu 
 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM ( Bara) Ndugu Christina Mndeme  akiwaongoza wanachama wa CCM na wananchi kucheza muziki wa Chama kutoka bendi ya TOT kwenye viwanja vya Nyamilangano.Chama Cha Mapinduzi kimezindua rasmi kampeni zake katika jimbo la Ushetu terehe 26 Septemba 2021.(Picha na Adam Mzee/ CCM Makao Makuu)


 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad