HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 1, 2021

CANADA YAIHAKIKISHIA NEEMA TANZANIA

 

 Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma

Serikali ya Canada imeahidi kuisaidia Tanzania katika kuimarisha Sekta ya Afya, Elimu na Mazingira kutokana na ufanisi katika usimamizi wa fedha katika miradi inayotekelezwa nchini kwa ushirikiano wa Serikali hiyo.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba wakati wa mkutano wake na Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Mhe. Pamela O’Donnell, ulioangazia ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Dkt. Nchemba alisema kuwa Sekta ambazo Serikali ya Canada imeahidi kuzisaidia zinaumuhimu mkubwa katika maendeleo ya nchi kwa kuwa pia ni sekta za kipaumbele katika Serikali ya Awamu ya Sita.

Alisema kuwa Tanzania na Canada zitaanzisha mazungumzo mapya ya namna ya kuendeleza programu za maendeleo zilizokuwa zikifadhiliwa na Serikali ya Canada baada ya progamu iliyokuwepo kumaliza muda wake mwezi Juni, 2021.

Aidha alisema kuwa Canada imeisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya Sekta ya madini, elimu, afya na utawala bora yenye thamani ya takribani dola bilioni 2.39 tangu Tanzania ilipopata uhuru.

Waziri wa Fedha na Mipango amemshukuru Balozi huyo wa Canada kwa kutambua juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi bora unaotambuliwa Duniani kwa kuimarisha uhusiano wa kimataifa.

Kwa upande wake Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Mhe. Pamela O’Donnell, alisema kuwa kuna mafanikio makubwa ambayo yamepatikana katika miradi mbalimbali iliyotekelezwa nchini Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Canada hususani katika Mfuko wa Afya na Elimu, ambapo fedha zilizotolewa zimetumika kikamilifu katika masuala yaliyokusudiwa.

“Kutokana na jitihada za Serikali katika kutekeleza miradi, tunaona kuna fursa ya kuendeleza ushirikiano katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya na kuwajengea uwezo wanawake”, alisema Mhe. Balozi Pamela O’Donnell.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiagana na Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamel O’Donnell, baada ya mazungumzo, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa tatu kulia) na Balozi wa Canada nchini, Mhe. Pamel O’Donnell, (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wizara pamoja na ujumbe wa Ubalozi wa Canada nchini baada ya mazungumzo yaliyofanyika, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Canada nchini, Mhe. Pamel O’Donnell, baada ya mazungumzo, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dk. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo, wakati wa mkutano kati yake na Balozi wa Canada nchini, Mhe. Pamel O’Donnell, ulioangazia masuala ya ushirikiano, jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaabani, akifafanua jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Balozi wa Canada nchini, Mhe. Pamel O’Donnell, jijini Dodoma.
Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamel O’Donnell, akizungumza wakati wa mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (hayupo pichani), ambapo Canada imeahidi kuisaidia Tanzania kuimarisha sekta ya afya, elimu na mazingira, katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiishukuru Serikali ya Canada kwa mchango wake katika sekta za maendeleo, wakati wa mkutano na Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamel O’Donnell, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bi. Amina Khamis Shaabani na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Bw. Melckzedeck Mbise, jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad