Na John Mapepele
WIZARA
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya
Afya imeratibu zoezi la hiari kwa wadau wa sekta hizo kupatiwa chanjo ya
Uviko-19.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi,
ameeleza kuwa makundi hayo yamependekezwa kupewa kipaumbele kwa
kuzingatia, pamoja na mambo mengine, umuhimu wao kwa jamii na ukweli
kwamba kwa mazingira ya kazi zao, wako katika hatari ya kuambukizwa.
“Shime
kwao kujitokeza siku ya Alhamisi na Ijumaa wiki hii Ukumbi wa Karimjee
Jijini Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi kwa hiari yao wale
waliojiandikisha katika Mabaraza na Idara zao husika,” amesema Dkt.
Abbasi.
Aidha, amesema kwa wale waliokosa kujiandikisha awali
wawe Wasanii au Wanahabari au Wanamichezo wajiandikishe mapema kupitia
namba 0654063274 au barua pepe matiko.mniko@basata.go.tz ya Kaimu
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Amefafanua kuwa Wasanii walio nje ya Dar es Salaam wataendelea kutumia utaratibu unaoendelea kutangazwa na Wizara ya Afya.
Ametoa
mwito kwa Wasanii, Wanahabari na Wachezaji kwa hiari yao kujitokeza na
kutumia fursa hii kipata chanjo ili kujikinga na kuwakinga wengine na
ugonjwa wa UVIKO 19.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akipata chanjo
katika Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam hivi karibuni baada ya
Rais Samia Suluhu Hassan kuizindua rasmi kitaifa
No comments:
Post a Comment