HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 16, 2021

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AONDOKA NCHINI KUELEKEA MALAWI


 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hii leo Agosti 16, 2021 ameondoka Nchini kuelekea Nchini Malawi kwaajili ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika kuanzia tarehe 17-18 Agosti, 2021.

Katika uwanja wa ndege wa Jijini Dodoma , Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan  amesindikizwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad