BenkiI
ya NMB, kupitia Program ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), imetoa msaada
wa viti na meza 150 kwa Shule Sekondari Saranga ya Kimara na Mashujaa ya
Sinza, pamoja na mabati 175 kwa Shule ya Msingi Mianzini, iliyopo
Magomeni Makurumla – zote wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam, vyote
vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 20.
Hafla
ya makabidhiano hayo imefanyika katika Shule ya Sekondari Saranga,
ambako Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo,
alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hheri James, mbele ya Mbunge wa
Ubungo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Kitila Mkumbo.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Bishubo alisema msaada huo ni sehemu ya
utaratibu wao wa kila mwaka, ambako hutumia asilimia moja ya faida yao
kwa mwaka uliotangulia, kurejesha kwa jamii kwa kusaidia utatuzi wa
changamoto zinazoikabili Sekta za Elimu na Afya, pamoja na majanga.
Bishubo
alibainisha kuwa, NMB inatambua, kuthamini na kuunga mkono jitihada za
Serikali katika kuboresha mazingira ya vijana na watoto wa Kitanzania
kupata elimu bora, hivyo wao kama wadau, wanao wajibu wa kusapoti
jitihada hizo kwa kusaidia kila penye uhitaji.
“Tangu
Januari mwaka huu hadi sasa NMB imetumia Sh. Bilioni 1.3 kutoa misaada,
ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam Peke yakep benki imetoa misaada yenye
thamani ya Sh. Milioni 207.9, kati ya hizo Sh. Mil. 144.5 katika elimu
na Sh. Mil. 93 Sekta ya Afya,” alisema Bishubo.
Kwa
upande wake, DC James, aliishukuru NMB, aliyoitaja kama sehemu ya
familia ya maendeleo wilayani mwake kutokana na ushiriki wao wa mara kwa
mara wa utatuzi wa changamoto katika elimu na afya, huku akiwataka
walimu na wanafunzi kutunza misaada hiyo, ili idumu kwa muda mrefu.
“NMB
wamekuwa wanafamilia wa maendeleo Ubungo, tangu siku naapishwa walikuwa
na sisi, naanza kazi NMB ilikuwa pamoja na sisi, tuliposimama
kuhangaika na changamoto za sekta ya elimu na afya, NMB iko pamoja nasi.
Wao wako na sisi katika raha na shida.
Naye
Waziri Mkumbo, aliishukuru NMB kwa namna inavyosaidia jamii
inayoizuguka na kwa kuhakikisha wanaendelea kutatua changamoto
mbalimbali zinazozikabili jamii.
Mkuu
wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo (kushoto),
akikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James (katikati) na
Mbunge wa Ubungo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo
(wa pili kulia), sehemu ya msaada wa viti na meza 150 kwa Shule za
Sekondari Saranga ya Kimara na Mashujaa ya Sinza, pamoja na mabati 175
kwa Shule ya Msingi Mianzini, iliyopo Magomeni Makurumla wilayani
Ubungo, jijini Dar es Salaam, vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 20.
Mkuu
wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo (kushoto),
akikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Khery James (katikati) na
Mbunge wa Ubungo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo,
sehemu ya msaada wa viti na meza 150 kwa Shule za Sekondari Saranga ya
Kimara na Mashujaa ya Sinza, pamoja na mabati 175 kwa Shule ya Msingi
Mianzini, iliyopo Magomeni Makurumla za wilayani Ubungo, jijini Dar es
Salaam, vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 20.
Mkuu
wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo (wa pili
kushoto) na Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio,
wakikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James, sehemu ya msaada
wa viti na meza 150 kwa shule za Sekondari Saranga ya Kimara, Mashujaa
ya Sinza, pamoja na mabati 175 kwa Shule ya Msingi Mianzini, iliyopo
Magomeni Makurumla za wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam, vyote
vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 20. Katikati wanafunzi wa Shule ya
Sekondari Saranga, Patrick Ndikwege na Vivian Valentino wakifurahia,
hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Saranga. Kulia ni Mbunge
wa Ubungo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo, (Na
Mpiga Picha Wetu).
……………………………………………………………………………
No comments:
Post a Comment