Naibu waziri wa Nishati azindua REA awamu ya Pili mzunguko wa Tatu Manyara - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 16, 2021

Naibu waziri wa Nishati azindua REA awamu ya Pili mzunguko wa Tatu Manyara

 

 Na John Walter -Manyara 

Naibu waziri wa Nishati mheshimiwa Stephen Byabato ameliagiza shirika la Umeme nchini (TANESCO)  mkoani Manyara kuwaunganishia Umeme wananchi wote Waliolipia gharama zinazohitajika kabla ya mwezi Agosti kuisha. 

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Wananchi katika Kata ya Tumati kijiji cha Mongahay wilayani Mbulu Kwenye hafla ya kuzindua na kuwashwa Umeme katika eneo hilo ikiwa ni mradi wa usambazaji wa Umeme vijijini (REA)  awamu ya tatu mzunguko wa pili.

Amesema serikali haitomvumilia mkandarasi au kiongozi wa Tanesco atakaekwamisha shughuli ya kuwapatia wananchi nishati ya Umeme.

Amesema agizo la serikali gharama za Umeme mkubwa ni shilingi 139,500 na Umeme mdogo ni shilingi 27,000 na atakaekiuka atachukuliwa hatua stahiki. 

Katika hatua nyingine amewataka viongozi kuendelea kuwasisitiza wananchi kujitokeza kulipia gharama hizo ili kupatiwa huduma.

Mkuu wa wilaya ya Mbulu  Sezaria Makotha amesema Vijiji 48 vya wilaya hiyo Kati ya Vijiji 110 vimeshapata Umeme ikiwa ni jitihada za ufuatiliaji wa karibu wa meneja wa Tanesco Mbulu Mhandisi Faustina Tuyaa.

Aidha Vijiji 71 vilivyobaki katika wilaya ya Mbulu vimeingizwa katika mpango wa awamu hii ili kutimiza adhma ya serikali ya kufikisha Umeme katika vijiji  pamoja na vitongoji vyote nchini ifikapo mwaka 2022.

Mbunge wa Mbulu vijijini Flatey Massay  ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwasogezea wananchi huduma hiyo ambayo itawawezesha kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji huku akiomba tatizo la mita za luku lifanyiwe Kazi na bili iwe tofauti na mjini.

Meneja wa Tanesco wilayani humo Faustina Tuyaa ameahidi kusimamia kikamilifu wakandarasi wanaotekeleza mradi huo ili ukamilike kwa wakati uliokusudiwa.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad