HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 18, 2021

MBIO ZA UHURU MARATHON KUJA KIVINGINE

 Mratibu wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon), Innocent Melleck (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza mbio hizo kwa mwaka huu, zinazotarajiwa kufanyika Desemba 9, 2021, jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Mshauri wa Ufundi wa Uhuru Marathon na Katibu wa Shirikisho la Riadha (mstaafu), Suleimani Nyambui (wa pili kushoto), Mtaribu Mwenza wa Uhuru Marathon, Revocatus Rugumila (kulia) pamoja na Mratibu wa Washirika wa Uhuru Marathon, Magdalena Gisse.
Mratibu wa Mbio za Uhuru (Uhuru Marathon), Innocent Melleck (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza mbio hizo kwa mwaka huu, zinazotarajiwa kufanyika Desemba 9, 2021, jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Mshauri wa Ufundi wa Uhuru Marathon na Katibu wa Shirikisho la Riadha (mstaafu), Suleimani Nyambui (kushoto) na kulia ni Mtaribu Mwenza wa Uhuru Marathon, Revocatus Rugumila.
Mshauri wa Ufundi wa Uhuru Marathon na Katibu wa Shirikisho la Riadha (mstaafu), Suleimani Nyambui (wa pili kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye hoteli ya Kebby's, jijini Dar es salaam, juu ya mbio za Uhuru Marathon zinazotarajiwa kufanyika Desemba 9, 2021.
 
 ============

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

MBIO za Uhuru Marathon mwaka huu zinatarajiwa kufanyika tarehe 9, Desemba 2021 katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam, zikiwa na lengo la kuenzi tunu za Taifa la Tanzania ambazo ni Umoja, Utaifa na Mshikamano ulioasisiwa na Waasisi wa taifa hili.

Mbio za mwaka huu zinafanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania, pia kuunganisha vijana wa Kitanzania na wenye uzalendo kuhakikisha kuwa na Mbio zenye ubora na vinavyokidhi vigezo vya taifa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mratibu wa Mbio hizo, Innocent Melleck amesema Mbio hizo kubwa zaidi nchini na barani Afrika kiujumla zitashirikisha Watanzania wa rika zote, ametoa rai kwa Mashirika mbalimbali na mtu mmoja mmoja nchini kuunga mkono mbio hizo ili zifanikiwe malengo yake.

Pia amesema Mbio hizo zina lengo la kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuhakikisha tunaenzi, kutunza na kuendeleza tunu za Taifa la Tanzania ambazo ni Umoja, Mshikamano na utaifa.

“Pamoja na hayo tupo katika hatua nzuri za kumuomba Mhe. Rais Samia kuwa mlezi wa mbio hizi ambazo zimebeba nembo na tunu za Taifa letu, Tunaimani kwa namna ambavyo Mama Samia amekuwa mchapa kazi na mzalendo atakubaliana nasi katika kufanikisha jambo hili muhimu kwenye Taifa letu”, amesema Innocent.

Pia ameeleza kuwa Taifa la Tanzania litaendelea kuwa na umoja na mshikamano ikiwa sambamba na kuendeleza mchezo wa Riadha nchini kutokana na kuwa mchezo ambao unaliletea taifa heshima kuleta ikiwa kuleta Medali mbalimbali katika nyanja za Kitaifa na Kimataifa (Olimpiki, Jumuiya ya Madola na Mshindano mengine ya Afrika.

Amesema mbio hizo kwa mwaka huu zitakuwa kama ifuatavyo:-

a. 42 km Wanawake na wanaume
b. 21km wanaume na wanawake
c. 10 Km wanawake na wanaume
d. 5 km wanawake na wanaume
e. 3 km (Mbio maalum za viongozi)
f. 2.5 km mbio za Watoto.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad