Wawezeshaji Uchumi wakiendesha baiskeli zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika
la Family Health International (FHI 360) limetoa msaada wa Baiskeli
242 kwa Wawezeshaji uchumi (Empowerment Workers) ngazi ya kata ili
kuwafikia wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya
maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
Hafla
fupi ya makabidhiano ya Baiskeli hizo imefanyika leo Jumatatu Agosti
16,2021 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni
rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati.
Akipokea
baiskeli hizo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati
amelipongeza Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia
mradi wa EPIC, wafadhili wa mradi USAID na PEPFAR pamoja na asasi za
kiraia kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuchangia na kusaidiana na
serikali katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa makundi yaliyoko
kwenye athari za kupata maambukizi ya VVU hasa mabinti.
“Wawezeshaji
kiuchumi nendeni mkafanye kazi kwa niaba ya serikali. Kafanyeni kazi ya
kuwafikia mabinti ili tupunguze maambukizi ya VVU katika jamii
yetu,toeni elimu ya miundo na uchumi ili wasichana wafanye kazi na
kupata mitaji na kupunguza tabia hatarishi za kupata maambukizi ya VVU”,amesema Dkt. Sengati.
Amesema
kwa mujibu wa Tanzania HIV Impact Survey ,2016-17, takwimu zinaonesha
hali ya maambukizi ya VVU kwa wasichana balehe na wamama vijana ni
asilimia 15.3% ukilinganisha na umri wao huo ambao ni asilimia 6.6%.
“Pia
kwa mujibu wa Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya Tanzania na Utafiti wa
Kiashiria cha Malaria, 2015 - 16 takwimu zinaonesha asilimia 27 ya
wasichana balehe wenye umri wa miaka kati ya 15-19 wamepata mtoto au
ujauzito”,ameeleza.
“Kutokana
na takwimu hizo inaonesha ni jinsi gani wasichana balehe na wamama
vijana wako katika athari kubwa na wanapaswa kulindwa na kuhakikisha
tunapunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI miongoni mwao”,ameongeza Dkt. Sengati.
Mkuu
huyo wa mkoa ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha
yanaifikia jamii na kutoa eleimu ya kutosha ili kupunguza changamoto
zinazowakumba wasichana zikiwemo mimba za utotoni,ukatili wa kijinsia na
maambukizi ya VVU na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nao ili
kuwa na jamii inayomthamini mtoto wa kike na kumpa ulinzi wa kutosha.
“Serikai
tunatambua na kuthamini mchango wa wadau na hatuwezi kufanya kila kitu
ndiyo maana nyinyi kama wadau mko mstari wa mbele kuisaidia serikali
kutekeleza agenda ya maendeleo ya 2030 na kuhakikisha kwamba 95-95-95
(95 % ya watu wanaoishi na VVU wanajua hali yao ya maambukizi, 95% ya
waliopima wameanza kutumia dawa na 95% ya walioanza dawa wamepunguza
makali ya VVU”, amesema Dkt. Sengati.
Akikabidhi
baiskeli 24 kati ya 242 Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt.
Shinje Msuka amesema Shirika la Family Health International (FHI 360)
limetoa baiskeli hizo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa
Kimataifa wa EPIC kwa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa
kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) na Shirika la Marekani la Maendeleo ya
Kimataifa (USAID).
“Kupitia
mradi huu tumetoa jumla ya baiskeli 242 kwa mkoa wa Shinyanga ambazo
zinagawiwa kwa walengwa katika halmashauri 5 za wilaya ambazo ni
Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Kahama, Ushetu na Msalala. Leo
tumekusanyika hapa kwa dhumuni la kugawa baiskeli kwa wawezeshaji uchumi
24 wa Manispaa ya Shinyanga”,amesema Dkt. Msuka.
Ameeleza
kuwa baiskeli hizo zitasaidia Wawezeshaji Kiuchumi kuwafikia wa
wasichana balehe na wamama vijana na kuchangia jitihada za serikali
katika kuhakikisha maambukizi ya VVU/UKIMWI yanapunguzwa na kufikia
malengo ya 95-95-95.
“Baiskeli
hizi ni sehemu ya vitendea kazi kwa wawezeshaji uchumi,tunaamini
zitapunguza changamoto ya usafiri na kuwawezesha kuwafikia wasichana
wengi zaidi katika kata, vijiji,vitongoji na hata ngazi ya kaya”,amesema
Dkt. Msuka.
“Baiskeli
hizi zinapaswa kutumika kwa matumizi ya mradi tu na si vinginevyo ili
kuboresha hali ya mabinti na kutokomeza janga la UKIMWI. Tanzania bila
UKIMWI inawezekana, tuendelee kutoa elimu kwa kila mtu asimame katika
nafasi yake kufikia na kuendeleza udhibiti wa janga la VVU/UKIMWI nchini
Tanzani”,ameongeza Dkt. Msuka.
Dkt.
Msuka amesema Mradi wa EPIC unatekeleza afua za utoaji wa huduma
zinazohusiana na VVU zikiwalenga makundi maalumu na yanayohitaji kupewa
kipaumbele ikiwemo wasichana wa rika balehe na wamama vijana, wanaume na
wanawake walio katika hatari ya kupata maambukizi ya VVU.
Amefafanua
kuwa Mpango wa DREAMS ni kati ya afua zinazotekelezwa na mradi wa EPIC
wenye lengo la kupunguza maambukizi ya VVU kwa wasichana balehe na
wanawake vijana wenye umri wa miaka 9 hadi 24, wanaoishi katika
mazingira hatarishi na wanafanya ngono katika umri mdogo ili waweze
kumudu gharama za maisha.
“Mradi
wa EPIC unatekeleza mpango wa DREAMS katika halmashauri 6 za mkoa wa
Shinyanga tangu mwezi Februari 2020 kupitia mashirika manne ya kijamii
ambayo ni Rafiki SDO, TADEPA, HUHESO Foundation na SHIDEPHA. Tayari
jumla ya wasichana 100,000 wamefikiwa.
“Wasichana
20,000 wamefikiwa na huduma za kitabibu kama upimaji wa VVU kwa
hiari,uchunguzi wa ukatili wa kijinsia,huduma za uzazi wa
mpango,uchunguzi wa magonjwa ya zinaa na huduma za dawa kinga (PREP),
38,000 wamefikiwa na huduma za miundo ambako wanaweka akiba na kukopa,
13,000 wameweza kuanzisha biashara zao wenyewe na 100,000 wamefikiwa na
huduma za mabadiliko ya tabia”,ameongeza.
Akizungumza
kwa niaba ya Wawezeshaji Uchumi,Sophia Chamba amelishukuru Shirika la
FHI 360 na Mradi wa EPIC kwa kuwapatia baiskeli hizo ambazo watazitumia
kuifikia jamii kutekeleza majukumu yao ambayo ni pamoja na kuwafundisha
mabinti balehe na wanawake vijana masomo ya uchumi na yanayosaidia
kujikinga na maambukizi mapya ya VVU.
Ameyataja
majukumu mengine kuwa ni kutoa elimua ya mabadiliko ya tabia na upimaji
wa VVU kwa kushirikiana na waelimisha rika,kufundisha masuala ya
ujasiriamali na kuandikisha mabinti balehe na wanawake vijana katika
vikundi kulinga na umri wao.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza leo Jumatatu
Agosti 16,2021 wakati akipokea baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa
Wawezeshaji uchumi (Empowerment Workers) ngazi ya kata ili kuwafikia
wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi
ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza wakati akipokea baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa
Wawezeshaji uchumi (Empowerment Workers) ngazi ya kata ili kuwafikia
wasichana balehe na wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi
ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga.
Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka akizungumza leo Jumatatu Agosti 16,2021 wakati akikabidhi baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa
Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na
wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani
Shinyanga.

Katibu
Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akizungumza wakati wa
hafla fupi ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa
Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na
wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani
Shinyanga.
Mwezeshaji
Uchumi,Sophia Chamba akilishukuru Shirika la FHI 360 na Mradi wa EPIC
kwa kuwapatia baiskeli hizo ambazo watazitumia kuifikia jamii kutekeleza
majukumu yao.
Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Shinyanga Geofrey Mambo akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akikagua baiskeli moja kati ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa
Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata ili kuwafikia wasichana balehe na
wamama vijana katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI mkoani
Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiendesha baiskeli ambayo kati ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa

wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi
baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Rachel Manga (kulia). Kushoto ni Meneja
wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary. Hizi ni sehemu ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi
baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Amina Bundala (kulia). Kushoto ni Meneja
wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary. Hizi ni sehemu ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi
baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Elizabeth Sollo (kulia). Kushoto ni Meneja
wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary. Hizi ni sehemu ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi
baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Yasinta Moses (kulia). Kushoto ni Meneja
wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati (wa pili kushoto) akikabidhi
baiskeli kwa Mwezeshaji Uchumi, Mary Ford (kulia). Kushoto ni Meneja
wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Shinyanga Dkt. Shinje Msuka, Wa pili kulia ni
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary. Hizi ni sehemu ya baiskeli 242 zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya baiskeli zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia Mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya baiskeli zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Wawezeshaji Uchumi wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya kukabidhiwa baiskeli zilizotolewa na Shirika la Family Health International (FHI 360) kupitia mradi wa EPIC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR kwa Wawezeshaji uchumi ngazi ya kata mkoani Shinyanga.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments:
Post a Comment