


Na Mwandishi Wetu, Morogoro
MFUKO
wa kuendeleza makandarasi wazalendo Contractors Assistance Fund (CAF),
umeendelea kuimarika na sasa unauwezo wa kukopesha makandarasi hao hadi
shilingi milioni 100.
Hayo
yamesemwa leo mkoani Morogoro na Naibu Msajili wa Bodi ya Usajili wa
Makandarasi (CRB) Mhandisi David Jere, kwenye mkutano wa mafunzo wa siku
tatu kwa makandarasi.
Alisema
CRB ilianzisha mfuko huo miaka ya hivi karibuni kwaajili ya kuwakopesha
makandarasi kwaajili ya kuanza kazi mara moja wanapopata miradi na
walianza na shilingi milioni 50 tu.
“Kwa
sasa mfuko wa makandarasi umeendelea kuimarika na una uwezo wa
kuwakopesha kila mmoja hadi sh milioni 100 kutoka shilingi milioni 50
za awali hivyo hii ni fursa kwenu ukiwa na sifa unakopeshwa unaanza
kazi,” alisema
Akifungua
mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya CRB, Mhandisi Consolata Ngimbwa
aliwataka makandarasi kuungana na kuanzisha chama kimoja chenye nguvu
ambacho kitakuwa sauti yao wanapokuwa na shida za kuwasilisha
serikalini.
Alisema
watu wa tasnia mbalimbali kama wahandisi, wasanifu majengo, wakadiriaji
majenzi na hata waendesha boda boda wanavyama vyao ambavyo vina nguvu.
“Kila
siku tunazungumzia suala hili hili sijui tumekwama wapi sasa naomba
ifike wakati tuseme inatosha, muwe na chama chenu chenye nguvu tusiwe
tunazungumza jambo hili hili kila tukikutana,” alisema
“Wakati
serikali ilipoamua kutumia force account tuliyumba sana na nilidhani
tumejifunza kwa yaliyotokea wakati huo kwamba ungekuwa wakati mwafaka wa
kukutana na kujadiliana namna ya kuwa na sauti moja lakini naaona
bado,” alisema.
Pia
aliwataka makandarasi hao kuacha kuomba zabuni kwa bei ya chini ili
kuwavutia watoaji wa zabuni kwani uzoefu unaonyesha wanapozipata
wamekuwa wakishindwa kuzikamilisha na wengine kukimbia.
Alisema
baadhi ya makandarasi wamekuwa wakijaza hela ndogo kama mbinu ya
kushinda zabuni lakini wanapopata kazi hizo wanashindwa kuzikamilisha
kwa wakati na wengine kushindwa kuzikamilisha kabisa.
“Jazeni
zabuni vizuri tena kwa uhalisia msijaze tu ilimpate zabuni lakini
mwishowe zinawashinda, hapa katikati tuliyumba sana baada ya serikali
kuanza kufanyakazi zake kwa kutumia utaratibu wa force account sasa
tumeanza kupata kazi za serikali tusifanye makosa, tuzifanye kwa weledi
mkubwa,” alisema Ngimbwa.
Alisema
CRB iliamua kuanza kutoa mafunzo hayo kwa makandarasi baada ya lawama
nyingi kwamba makandarasi hao wamekuwa wakiweka bei ambazo hazina
uhalisia.
Mhandisi
Ngimbwa aliwasisitiza pia kufanyakazi kwa ubia na makandarasi wenzao na
wanaposhindwa kujua namna ya kuzifanya wafike ofisi za bodi hiyo au kwa
wataalamu kwaajili ya kuelekezwa namna ya kufanyakazi za aina hiyo.
“Wengi
tunaingia kwenye kazi za ubia lakini tunashindwa sijui kwasababu
hatuzijui au, uzuri wa kazi hizi ni kwamba mnaunganisha nguvu na kufikia
vigezo vinavyohitajika na kama mkishindwa njooni CRB mtaelekezwa,”
alisema
Mratibu
wa Mafunzo wa CRB, ambaye ni Msanifu Majengo, Neema Fuime alisema
mafunzo hayo ya mara kwa mara yanalenga kuwapa makandarasi wa ndani
uwezo wa kujaza zabuni kitaalamu wanapoomba kazi.
Alisema
awali baadhi ya watoa kazi walikuwa wakilalamika kuwa makandarasi wengi
hawana uwezo wa kujaza zabuni ndiyo sababu CRB ikachukua jukumu la
kuwapa mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment