*Wananchi baada kulipa kupitia mkopo wa Benki kumiliki nyumba ndani ya siku moja.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WAZIRI
wa Ardhi, Nyumba na Makazi William Lukuvi amefurahishwa na ubunifu wa
ujenzi wa nyumba bora na gharama nafuu unaofanywa na Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC) ambao umeanza kwa awamu hii ambapo wameanza kujenga
nyumba 400 mkoani Dodoma.
Akizungumza
mara baada ya kutembelea banda la NHC kwenye Maonesho ya 45 ya
Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere
Jijini Dar es Salaam Waziri Lukuvi amesema kwa mara ya kwanza ubunifu
huo utawezesha mkopaji kupata mkopo na kupata nyumba kwa siku moja na
shirika la Nyumba wamewawezesha wananchi mkopo ambao utakuwa chini ya
asilimia 10.
Amesema
kuwa awali miradi ya Ujenzi ilikuwa inafanywa wakiwa watu wamelipa na
kuanza kusubiri nyumba huku wakiendelea kulipa fedha za kwa nyumba
waluzopanga.
Waziri Lukuvi amesema kazi ya NHC imeanza kuonekana katika kuwanufaisha wananchi nyumba za gharama nafuu.
"Mwananchi
atapewa mkopo benki atalipa Shirika la Nyumba na Shirika litampa
ufunguo wa nyumba na hati ya kumiliki kiwanja kwa siku moja". Amesema
Waziri Lukuvi.
Amewataka
wananchi kuzichangamkia nyumba zinazojengwa na NHC ambazo zipo mkoani
Dodoma ambazo Agasti Mwaka huu watazitoa kwa wananchi kwa utaratibu
maalumu.
"Tunataka
tuwaelekeze Real Estate Developers kama Shirika la Nyumba ndio mjenzi
kiongozi, kama kiongozi tunataka kutoa masomo mawili kwanza, kila
mwananchi anaeahidiwa au anaelipa kwaajili ya kupata nyumba lazima apate
nyumba mara baada ya kulipia badala ya utaratibu wa sasa mtu anatoa
Fedha ya kununua nyumba alafu hizohizo fedha zinatumika kufanya ujenzi
na mwananchi kuanza anadanganywa anapewa nyumba baada ya miaka miwili
au mitatu". Amesema Lukuvi.Waziri Lukuvi aipongeza NHC kwa ubunifu wa
nyumba za gharama nafuu.
Waziri
wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza mara
baada ya kutembelea Banda la Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) katika
maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanyoendelea kufanyika viwanja vya
Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam yanayoendela
Waziri
wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiangalia ramani ya
mradi wa Nyumba zilizojengwa Dodoma kwa ajili ya wananchi zenye gharama
nafuu wakaiti alipotembelea maonesho ya Sabasaba katika Banda la NHC.
Awesome and interesting article. Great things you've always shared with us. Thanks. Just continue composing this type of post.
ReplyDelete