TTCL YAWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO SABASABA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 4, 2021

TTCL YAWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO SABASABA

Baadhi ya wateja waliotembelea Banda la TTCL leo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam wakipatiwa huduma mbalimbali.

 

Meneja wa Banda la TTCL, Bw. Ramadhani Mshana (kulia) akimkabidhi simu Kaimu Meneja wa Utafiti na Mipango wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bw. John Fwalo mara baada ya kununua ndani ya banda la TTCL.

Meneja wa Banda la TTCL, Bw. Ramadhani Mshana (kushoto) akimkabidhi simu Afisa Mwandamizi Taarifa za Biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bi. Magdalena Shirima (kulia) mara baada ya kununua simu hizo ndani ya banda la TTCL kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limewakaribisha wananchi wanaotembelea Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam kutembelea Banda la TTCL kujipatia bidhaa na huduma mbalimbali za shirika hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ndani ya Banda namba 65 la TTCL, Meneja wa Banda la TTCL, Bw. Ramadhani Mshana alisema huduma zinazopatikana ndani ya banda la TTCL ni pamoja na kutoa bure line za simu (Simcard) kwa wateja zikiwa na MBs na dk na sms za kutosha kwa matumizi ya wiki nzima bure.

Alisema ili mteja anufaike na huduma hizo anatakiwa kuwa na kitambulisho cha taifa kwa kusajilia. Alizitaka taasisi binafsi na za Umma zinazohitaji kupatiwa huduma za call center na huduma za mkutano kwa njia ya Video (Video conference) kutembelea banda la TTCL kupata suluhisho ya huduma hizo, pamoja na huduma za kuunganisha wateja wa simu na intaneti kwa njia za Copper, Fiber, na Microwaves (Radio).

"Bidhaa zingine zinazopatikana ndani ya banda letu ni pamoja na Vifaa vya 'wireless internet' kama MiFi, Router, Dongle, Wingle Simu za mezani za Wireless maarufu kama FWT, Router mpya ya kisasa kabisa ambayo ina uwezo wa kuunganishwa na simu ya mezani (kichwa cha simu). Hii ni kwa matumizi ya ofisi na majumbani Kadi za malipo N-card, alisema Meneja wa Banda la TTCL, Bw. Ramadhani Mshana.
Baadhi ya wateja waliotembelea Banda la TTCL leo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam wakipatiwa huduma mbalimbali.
Kushoto ni watoa huduma wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakihudumia wananchi waliotembelea Banda la TTCL leo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni mfanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) akimuhudumia mmoja wa wateja waliotembelea Banda la TTCL leo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watoa huduma na wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) akipata picha ya kumbukumbu mbele ya Banda la TTCL kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad