HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 23, 2021

TAKUKURU MKOANI PWANI YAWASHITUKIA MATAPELI WANAOJIFANYA MAOFISA WA TAASISI HIYO

 Na Victor Masangu, PWANI

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Pwani imewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya matapeli wanaojifanya ni maofisa wa Taasisi hiyo ili waweze kuchukuliana hatua Kali za kisheria.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzana Raymond ametoa tahadhari hiyo akitoa taarifa ya utendaji kazi wa miezi mitatu kwa waandishi wa habari.

Suzana alisema wapo wanachi wamekuwa wakipigiwa simu na watu wanaodaiwa kuwa ni matapeli wakitakiwa kufika kwenye ofisi za TAKUKURU na wanapofika hapo hakuna taarifa za wito wao.

Aidha Suzana ameongeza kuwa katika kipindi cha miezi mitatu kutoka April hadi June wamepokea malalamiko 127 kati ya hayo 57 uchunguzi wake unaendelea na 70 hayahusiani na Taasisi hiyo.

Alisema katika kipindi hicho kesi 15 ziliendelea kuendeshwa katika mahakama mbalimbali za mkoa wa Pwani na kwa miezi hiyo mitatu kesi sita zilitolewa maamuzi na Jamhuri ilishinda na washitakiwa walitakiwa kulipa faini au kutumikia kifungo.

Pia katika hatua nyingine aliwahimiza wananchi wote wa mkoa wa Pwani kuhakikisha wanawafichua watu wote ambao wanavunja Sheria kwa kujifanya wao ni watumishi wa Takukuru.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Raymond akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na wimbi la baadhi ya watu ambao wanajifanya maafisa wa Takukuru.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad