HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 7, 2021

Njombe:CCM wasisitiza kuchukua tahadhari dhidi ya Corona

 Na Amiri Kilagalila,Njombe

CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe kimetaka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID 19 kwa kuzingatia usafi,kuvaa barakoa ,utumia vipukusi na kuepuka mikusanyiko.

Akizungumza na wandishi wa habari katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole amesema Corona ipo nchini kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alivyoagiza hivyo kila mwananchi achukue tahadhari.

"Rais ametuelekeza juu ya ugonjwa wa Corona,lazima niwaambie ndugu zangu hata Njombe kuna Corona na serikali imekuwa wazi tuchukueni tahadhari"alisema Erasto Ngole

Aidha bwana Ngole akizungumzia swala la katiba pya amesema siyo kipaumbele cha serikali ya awali ya sita ambapo  juhudi zinazofanyika ni kutatua changamoto zinazowakabili Watanzania kwa kusimamia miradi  ili Ilani itekelezwa kikamilifu.

"Katiba mpya sio kipaumbele cha watanzania kwa sasa wala sio kipaumbele cha serikali ya awamu hii.Kipaumbele ni kutatua changamoto zinazowakabili wananchi,tumejikita kutekeleza Ilani ya CCM ambayo ndio deni letu kwa wananchi,katiba mpya itakuja baada ya kupunguza mzigo wa changamoto unaowakabili watanzania"alisema Ngole 

Nae Mganga mkuu wa  Halmashauri ya Mji wa Njombe Isaya Mwasubila amesema serikali kupitia watalaamu wa afya wanaendelea kutoa elimu ya kujikinga na CORONA huku akiagiza maeneo ya ofisini na kwenye mikusanyiko kuhakikisha wanaweka ndoo za maji ya kunawa,kuvaa barakoa na kupaka vipukusi mikononi.

"Ni tahadhari ambazo zinaendelea kuchukuliwa ikiwemo na zile za awamu ya kwanza,pia kwenye awamu hii ya tatu hatua ni zile zile ikiwemo kunawa mikono kwa maji safi na tiririka pia kuepuka misongamano"Alisema Isaya Mwasubila

Baadhi ya wananchi waliozungumza na kituo hiki wamesema serikali kupitia watalaamu inatakiwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kujikinga na Corona kwa kuwa bado  kumekuwa na hali ya upuuziaji kati jamii dhidi ya kujikinga na Corona.

Vile vile Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe kimempongeza kwa dhati Rais Samia kwa kupokea kijiti katika mazingira magumu baada ya aliyekuwa Rais wa Tanzania Mh, John Pombe Magufuli kufariki dunia huku nchi ikiendelea kutulia.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad