Mfumo huo ni kutafuta masoko kwa Mazao 36
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shabaan amesema wafanyabiashara wana umuhimu mkubwa wa kuwa na mfumo wa taarifa za biashara kwa kuwa utawaletea tija na kuondoa changamoto zao katika katika utafutaji wa masoko .
Amesema lengo kubwa la mfumo huo ni kumrahisishia mfanyabiashara kupata taarifa sahihi ili aweze kufanya biashara yake kwa urahisi na kuondokana na urasimu uliokuwa kwa baadhi ya huduma zinazohusiana Biashara wakati wa unazihitaji kwa haraka.
Akizungumza katika uzinduzi wa mfumo wa taarifa za biashara uliozinduliwa viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya 45 yanayoendelea jijini Dar es Salaam Waziri Shabaan amesema mfumo huo utaleta tija kwa wafanyabiashara na kukuza uchumi kutokana na bidhaa kupata masoko ya nje ya nchi kiurahisi .
Amesema mfumo huo unatakiwa kwenda katika mabadiliko ya teknolojia kwani Teknolojia inabadilika kila Siku kwa Mamlaka inayosimamia mfumo huo.
Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe aliwataka wafanyabiashara kwenda na wakati na wafanye kazi kisasa kwa kutumia njia ya mtandao ambapo dunia ndiko iliko kwa sasa
Amesema biashara kwa njia ya mtandao inasaidia kurahisisha muda na hata kupata wateja wengi tofauti na njia iliyozoeleka.
Aidha Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade)Balozi Mteule Edwin Rutageruka alisema mfumo huo umeshirikisha bodi mbalimbali ikiwemo bodi ya mkonge,kahawa,na korosho ili ziweze kusaidia katika ukusanyaji wa taarifa.
Kagahe amesema Mfumo huo wa taarifa una Mazao 36 ambapo Tanzania Bara 30 na Zanzibar sita.
Amesema mfumo huo unaleta tija na ndio maana hivi sasa umeletwa TanTrade kwa kuwa wao ndio wadau wakubwa wa wafanyabiashara.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Shaaban Said Omary na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kagahe wakibonyeza kitufu kuashilia uzinduzi Mfumo wa Taarifa za Biashara kwa njia ya Mtandao (Trade Portal) uliofanyika viwanja katika Maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Shaaban Said Omary akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa taarifa za Biashara (Trade Portal) uliozinduliwa katika Maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea kufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kagahe akitoa maelezo kuhusiana na Mfomo wa Taarifa za biashara katika Mtandao (Trade Portal) uliozinduliwa katika Maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea kufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mkuu wa Mamlaka Biashara Tanznia (Tantrade) Balozi Mteule Edwin Rutageruka akitoa taarifa kuhusiana na kuanzisha Mfumo wa Taarifa za Biashara kwa njia ya mtandao (Trade Portal) uliozinduliwa katika Maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea kufanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau walioshiriki katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja ya Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Shaaban Said Omary na Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Exaud Kagahe na makundi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa Mfumo wa Taarifa za biashara kwa njia ya Mtandao (Trade Portal).
No comments:
Post a Comment