
Mhandisi Mkazi wa Mradi wa Uzalishaji Umeme wa Maji wa Julius Nyerere, Eng. John Mageni akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati ujumbe wa benki hiyo ulipotembelea mradi huo unaofanyika katika bonde la mto Rufiji. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme, Eng. Pakaya Daniel na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati) akiteta jambo na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme, Eng. Pakaya Daniel wakati ujumbe wa benki hiyo ulipotembelea mradi huo unaofanyika katika bonde la mto Rufiji. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay.

No comments:
Post a Comment