Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Bayama Orphanage and Community Service (BOACSE) Tanzania imeingia katika ushirikiano usiokuwa wa kikomo Shirika la Basic Internet Foundation la nchini Norway kwa lendo la kuwezesha vifaa na ufundishaji matumizi ya hudua ya internet katika shule za sekondari mkoani Songwe.
Ushirikiano huo wa BOACSEA ulifikia hatua ya hutoaji huduma hiyo mashuleni baada ya kuona changamoto ya ukosekanaji wa huduma hiyo kwa shule hizo zilizopo vijijini.
Mkurugenzi wa BOACSE,Emmanuel Mahenga alisema mlengo wa taasisi yake ni kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ikiwa ni kuwapatia mahitaji muhimu ya kibinadamu,lakini baada ya kubaini changamoto ya huduma ya habari mawasiliano (ICT) shuleni ili kuwa raisi kuongea na wadau na kuweza kukubaliana kusaidia huduma hizo mashuleni.
Alisema ushirikiano wa kubaliano wa bila kikokomo kwa mkoa wa songwe ni kusaidianshule za vijijini mkoani humu kupata huduma hizo ilikuendana na mlengo wa serikali kuhakiki shule zinafaidika na huduma za matumizi ya habari mawasiliano ICt ili kurahisisha hupatikanaji wa kiada na ziada katika ufundishaji.
"Takribani ni muda wa wa miaka miwili BOACSEA na Basic Internet Foundation kushirikiana amabapo kwa Songwe Uunganishwa wa huduma ya ICT umeshafanyika katika shule tano ambapo ni Jakaya kikwete,Chikanamlilo,Julius Nyerere,Sadocki Simwanza V.T.C na Nkangamo "alisema Mahenge na kuongeze.
Ushirikiano wa kutoa ujuzi wa kisasa wa ICT na maarifa kwa walimu na wanafunzi ili kuwezesha kukubaliana na changamoto wanakabiliana na mwendo wa ukuaji wa uchumi wa dunia.
Alisema taasisi yake inapenda kuwakaribisha wadau ilikuendelea kushirikiana kusaidia shule za sekondari za vijijini kuweza kuendana na kasi ili kujifunza,kupanua ubunifu wa walimu na wanafunzi wao kuendana na ushirikiano wa elimu duniani kote.
Seti ya vifaa vya mawasiliano ya intaneti katika shule ya sekondari ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo Tunduma mkoani Songwe.
Mratibu wa Taasisi ya BOACSE Tanzania Emmanuel Mahenge akifunga kifaa cha mawasiliano ya intanet katika Shule Sekondari ya Jakaya Kikwete iliyopo Tunduma mkoani Songwe.
No comments:
Post a Comment