HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 13, 2021

Waziri Mkuu afurahishwa na CRDB Bank Pamoja Bonanza kuhamasisha mshikamano, Bunge laibuka mbabe kwa kubeba kikombe cha jumla

Dodoma 12 Juni 2021 - Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa bonanza la michezo lililopewa jina la “CRDB Bank Pamoja Bonanza” ambalo pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kushiriki katika michezo na kujenga afya pia linalengo la kuhamasisha mshikamano kwa Watanzania na ushiriki katika shughuli za maendeleo.

Waziri Mkuu alisema bonanza hilo linatekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan ya kuwaleta Watanzania pamoja na kushirikiana katika shughuli za kijamii na uchumi wa Taifa letu.

“Mheshimiwa Rais katika moja ya hotuba zake alituasa tukitaka kwenda haraka twende peke yetu, lakini tukitaka kwenda mbali twenda pamoja. Asanteni Benki ya CRDB kwa kuonyesha mfano wa kutuleta pamoja Bunge, Wizara pamoja na Wananchi wote kupitia CRDB Bank Pamoja Bonanza,” alisema Waziri Mkuu.

Aidha, Waziri Mkuu alizitaka taasisi nyengine za umma na binafsi kuiga mfano wa Benki ya CRDB kwa kuandaa mabonanza kama hilo ilikuendelea kujenga utamaduni wa michezo na mshikamano miongoni mwa Watanzania. “Niwahamasishe na Watanzania kuendelea kushiriki katika michezo ili kuimarisha afya zetu,” alisisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema lengo kuu la kuandaa bonanza hilo ni kuisogeza benki hiyo karibu na Serikali, Bunge na Wizara, ili kupata nafasi ya kusikiliza mahitaji yaliyopo na kujua namna gani benki hiyo inaweza shiriki kikamilifu katika mipango ya maendeleo ya nchi. 

Naye Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dkt. Tulia Ackson aliiomba Benki ya CRDB kuendeleza utamaduni huo ambao wamekuwa nao kila mwaka Wa kushirikiana na Bunge katika kuhamasisha michezo na kujenga mahusiano. “Tunawapongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa bonanza hili kwa mara nyengine tena, hii ni njia nzuri sana ya kujenga mahusiano huku tukiimarisha afya zetu,” alisema Tulia.

“Miaka ya nyuma tulikuwa tukifanya bonanza hili na Bunge, mwaka huu tumeshirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kushirikisha Wizara zote. Malengo yetu mwakani ni kuhusisha muhimili mwengine wa Serikali kwamaana ya Mahakama,” aliongezea Nsekela.

Akikabidhi kombe na medali kwa mshindi wa jumla Benki ya CRDB, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul aliwapongeza washindi katika bonanza hilo na kuwashukuru watumishi wote wa Serikali, Bunge, Benki ya CRDB na wananchi waliojotokeza kushiriki katika bonanza hilo.

Katika CRDB Bank Pamoja Bonza, timu ya Benki ya CRDB iliibuka mshindi katika mpira wa miguu, timu ya Bunge iliibuka mshindi katika mpira wa kikapu na katika mpira wa pete timu ya Watumishi wa Wizara iliibuka mshindi. 

Vilevile kulikuwa na michezo mingine ya burudani ikiwamo kuvuta Kamba, kukimbia na magunia, kufukuza kuku, mchezo wa bao, karata, draft, pamoja na pool table. 




































No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad