Na Amiri Kilagalila,Njombe
Baada
ya jitihada kubwa zinazofanya na serikali katika kuvitangaza vivutio
vya utalii ndani na nje ,Huko mkoani Njombe jiwe la kushangaza lenye
ukubwa wa ekari 7.5 likiwa na umbo la ramani ya bara la Africa juu yake
huku muonekano wa nje wa jiwe zima ukiwa na umbo la ramani ya Dunia
limegeuka kivutio kikuu cha utalii mkoani humo na kusababisha mamia ya
watu kuendelea kufika katika kijiji cha Igodivaa wilayani Wanging'ombe
kujionea maajabu hayo ya kivutio hicho
Jiwe
hilo ambalo limepewa jina asilia la Lwivala likimanisha uangavu lina
mambo mengine matano yakustaajabisha ikiwa ni pamoja na kuwa na mkanda
wa mwamba ambao unadaiwa kuwa ni mlango wa kuzimu,Nyoka mkubwa asiye na
madhara kwa viumbe wengine,kochi asilia la kifalme,Kisima kilicho
katikati ya mwamba ambacho hakikauki kipindi chote cha mwaka pamoja na
viji mwamba vidogo vinavyo ng'ara kila ifikapo saa 12 asubuhi na jioni.
Kwa
mara ya kwanza Mwamba wa Lwivala ulitambuliwa 1996 na kutangazwa 2002
na mwenge wa uhuru kuwa kivutio cha utalii na kuanzia hapo maelfu ya
watu kwa nyakati tofauti waka anza kuzuru kujionea maajabu hayo ambapo
mingoni mwao ni Hannes Van Niekerk raia wa Afrika kusini,Helen Mlowe na
Justin Mligo ambao wameeleza namna walivyofurahia kutembelea kivutio
hicho.
"Kwanza eneo hili linavutia na kila mtu
atakayefika hapa tunaamini atavutiwa na mazingira haya,lakini inabidi
tuvitunze vifutio hivi,tumeona picha ya bara la Afrika juu ya jiwe
ambapo sijawhi ona maajabu kama haya"alisema Heln Mlowe
Ikielezwa
historia fupi ya jiwe hilo na Mzee wa mila ambaye pia ni muongoza
wageni Yuda Masamaki Mlowe na Sebastian Anania mwenyekiti wa kijiji cha
Igodivaa wanasema katika jiwe hilo ndipo walikuwa wanakutana zamani na
kuomba mambo mbalimbali na kujibiwa lakini kwasasa imekuwa ngumu
kwasababu ya shamabulio la tamaduni za magharibi.
"Siku
za nyuma tulikuwa tunaleta magari yakawa yanaingia mpaka huku kwa hiyo
maji yalizila na wenye mizimu yao kwa hiyo lazima tuhakikishe haya
tunayafanyia kazi"alisema Yuda Mlowe
Wakati
mwamko wa utalii ukizidi kukua kila uchwao lakini vivutio vingi vya mkoa
wa Njombe havijulikani jambo ambalo linamsukuma mkurugenzi wa kampuni
ya RAMIKA Safari's and Tours Michael Katona kujitosa huko na kuanza
kuvitangaza na kuhamasisha watu kutembelea
"Vivuti
vya ndani ya mkoa wa Njombe watu wengi wamekuwa hawavitambui na wengine
wanavishangaa kwa hiyo sisi wadau wa utalii ndani ya mkoa wa Njombe na
nyanda za juu kusini tumeona angalau sasa tuhamisishe jamii kuona
umuhimu wa hivi vivutio"alisema Michael Katona
Baadhi ya watalii wa ndani na wa nje wakiwa wamezunguka picha ya ramani
ya bara la Afrika ambayo ipo juu ya jiwe lenye ukubwa wa ekari 7.5
wakipewa maelekezo na msimamizi wa kivutio hicho wilayani Wanging'ombe
mkoani Njombe.Baadhi ya watalii wa wakiwa wamekaa kwenye mfano kochi la asili (Jiwe)
lilopo kwenye kivutio cha jiwe huku lenyewe likiwa na historia yake
katika kivutio hicho.Baadhi ya watalii wakipata maelekezo kabla ya kuanza kuzunguka kivutio cha jiwe la Lwivala mkoani Njombe.
No comments:
Post a Comment