HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 22, 2021

Vyama vya Siasa Kuendeleza Ushirikiano na Serikali, Vyawapongeza Rais Samia, Dkt. Mwinyi

 

Na Mwandishi Wetu ORPP
VYAMA vya Siasa nchini vya ahidi keendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambazo zinaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussen Ally Mwinyi, mtawalia.

Ahadi hiyo imetolewa juzi tarehe 20 Juni 2021 na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Magalle Shibuda kupitia Taarifa yake kwa umma akitoa maazimio ya Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza hilo kilichakaa tahere 3 Juni 2021 Jijini Dar es Salaam.

“Kamati kwa niaba ya Vyama vyote vya Siasa vyenye usajili wa kudumu ambavyo kimsingi vyote ni wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa, ili ahidi kushirikiana na Serikali zote mbili,Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuleta maendeleo ya Watanzania.” Ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha kupitia taarifa hiyo Kamati ya uongozi imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu kwa uamuzi wake wa kutaka kukutana na viongozi wa Vyama vya siasa nchini.

Katika hatua nyingine Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa kwa pamoja iliazimia kutoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Hussen Ally Mwinyi kwa kuwa Rais wa Zanzibar wa awamu ya nane kutokana na ushindi alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Baraza hilo limeendelea kutoa pongezi kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Hussen Ally Mwinyi kwa namna wanavyoendesha Serikali kwa kushirikisha vyama vya upinzani ambapo taarifa hiyo imeeleza kuwa hiyo ni ishara ya kudumisha Demokrasia ya Vyama vingi hapa nchini.

Baraza la Vyama vya Siasa ni chombo kinachoundwa chini ya kifungu 21B cha Sheria ya Marekebisho ya Vyama vya Siasa namba 7 ya Mwaka 2009 ambalo linashirkisha wajumbe wawili ambao ni viongozi wa kitaifa kutoka vyama vyote 19 vyenye usajili wa kudumu huku shughuli zake zikiratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad