SHOW YA DAVIDO YALENGA KUSAIDIA WATOTO YATIMA WA NCHI MBALIMBALI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 12, 2021

SHOW YA DAVIDO YALENGA KUSAIDIA WATOTO YATIMA WA NCHI MBALIMBALI

 Na.Khadija Seif,Michuzi Tv

PROMOTA maarufu nchini DMK ambae amekuwa akiandaa show mbalimbali nchini za wasanii hasa Muziki pamoja na Filamu  amewataka Mashabiki  wake kutazama show ya Msanii Davido kutoka Nigeria kupitia mtandaoni ili pesa zitakazopatikana zisaidie watoto yatima hapa nchini. 

 Aidha Dmk  ameeleza jinsi ya kutazama show hiyo inayokwenda kwa jina la "Global unity concert itakayofanyika nchini Nigeria  Juni 16 mwaka huu na kwa mara ya Kwanza Msanii Davido ataweza kutoa burudani Mubashara na itawapa fursa waliombali kuona show hiyo kwenye Mtandaoni wa shurtv.

"Show hiyo ya global unity concert utaweza kuiona Mubashara Mtandaoni kwahiyo kwa kupitia kiasi kidogo cha pesa utakacholipia kitakuwezesha kuchangia kabisa kwa watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu".

Hata hivyo Dmk amesema kutokana na yeye kuwa mzoefu kwenye tasnia ya burudani hasa kutafuta Masoko nje ya nchi hivyo tutegemee kuona show ya Zuchu,Alikiba pamoja na Mkali Diamond platinum hivi punde.

"Hivyo tupo kwenye Maongezi na Wasanii wa Nyumbani kwa Sasa na tupo bega kwa bega kutoa support Nyumbani kupitia wasanii wa Tanzania ila kwa Sasa tumeanza na mkali Davido na show itafanyika nchini Nigeria ."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad