RC MAKALLA AWAPA MATUMAINI MAPYA WAFANYABIASHARA SOKO LA MACHINGA COMPLEX - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 22, 2021

RC MAKALLA AWAPA MATUMAINI MAPYA WAFANYABIASHARA SOKO LA MACHINGA COMPLEX

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam kuja na Mpango Mkakati wa Kuendeleza na Soko la Machinga Complex ili Soko hilo liwe kimbilio kwa Wamachinga na Wateja.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea Soko hilo na kusikiliza kero za Wafanyabiashara sokoni hapo ambao wamemueleza sababu zinazopelekea Wafanyabiashara kulikimbia Soko hilo na kwenda mitaani.

Miongoni mwa Kero zilizotolewa na Wafanyabiashara hao ni mazingira mabovu ya kufanya biashara, Utaratibu mbovu wa kupata vizimba, Kodi kubwa, Sheria kandamizi, Ushirikiano mbovu wa Viongozi, Umeme, Maji, Vyoo, Maji taka, Miundombinu isiyorafiki na utaratibu wa kulipa Kodi ya mwezi badala ya Ushuru wa siku.

Kutokana na Malalamiko hayo RC Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Jiji kuhitisha vikao vya Mara kwa Mara na Wafanyabiashara hao na kupeana Mrejesho wa utatuzi wa kero zao ili mwisho wa siku biashara zifanyike na Serikali ipate Mapato.

Aidha RC Makalla ameelekeza Viongozi wa Soko hilo kuachana na tabia ya kufungia biashara za wapangaji wanaoshindwa kulipa Kodi na badala yake wakae mezani kuangalia namna Bora.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Halmashauri ya Jiji kufuatilia fedha za NSSF zilizotolewa Kama mkopo wa Ujenzi wa jengo hilo lili kujua Kama mkopo umemalizika au bado Deni lipo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad