Na Shukrani Kawogo, Njombe.
Timu
123 za mpira wa miguu wilayani Ludewa mkoani Njombe zimejitokeza
kushiriki ligi ya mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga
iliyozinduliwa hivi karubuni na kushirikisha kata zote 26 wilayani humo.
Akizungumzia
mashindano hayo mmoja wa wasimamizi wa ligi hiyo kutoka Katika chama
cha mpira wa miguu wilayani humo Jimmy Haule amesema mashindano hayo
yameanza vyema ambapo timu hizo ni kutoka katika vijiji vyote 77 vya
wilaya hiyo ambazo zinashiriki mashindano hayo.
Amesema kwa sasa
mashindano hayo yameanza katika hatua za makundi za vijiji ambapo timu
itayopata ushindi itaingia katika mchuano ngazi ya kata kisha tarafa na
hatimaye wilaya.
Amesema kuna baadhi ya kata mashindano hayo
yamekuwa yakisimamiwa na watendaji kata ambao wamekuwa wakiwasiliana nao
kwa ukaribu ili kujua endapo kuna changamoto zozote zinazojitokeza.
Sambamba
na hilo pia alielezea baadhi ya changamoto wanazo kabiliana nazo kuwa
ni kushindwa kuyafikia maeneo yote yanayoendeshwa michuano hiyo kutokana
na jografia ya wilaya hiyo na miundombinu isiyo rafiki.
"Tumekuwa
tukiwasiliana na wenzetu wanaoongoza mashindano katika kila kata lakini
changamoto kubwa inakuja ni jinsi ya kuyafikia maeneo kwani kunatokea
changamoto kutokana na jografia ya wilaya yetu pamoja na miundombinu
isiyo rafiki kwa kufika huko inapelekea kutofika kwa wakati hivyo
tunalazimika kuahirisha mechi mpaka tutakapotatua changamoto hiyo",
Alisema Haule.
Aidha kwa upande wa washiriki wa mashindano hayo
wamekiri kufurahishwa na michuano hiyo ambapo ni michuano ambayo
inaimarisha ushirikiano baina ya vijana sanjari na kufanya afya zao kuwa
bora zaidi.
Nasibu Luoga ni mmoja wa washiriki hao amesema kuwa
wana kila sababu ya kuwaletea mashindano hayo kwani ni makubwa na
yanayotumia gharama nyingi sana.
Amesema kuwa kuwaomba wadau
mbalimbali kujitokeza kwa wingi na kumuunga mkono mbunge huyo kwa kile
anachofanya ili kuweza kuimarisha mashindano haya."Tunaomba mjitokeze
wadau wengi zaidi ili kuunga mkono juhudi hizi zinazofanywa na mbunge
wetu katika kuongeza nguvu zaidi za kuimarisha vijana", Alisema Luoga.
Akizungumzia
mashindano hayo mbunge huyo amesema kuwa katika kufanikisha mashindano
hayo ametoa jezi seti 140 pamoja na mipira 140 vyenye thamani ya
shilingi Milioni 28.
Amesema mashindano hayo yatakapo kamilika Katika
ngazi ya kata timu itakayoibuka mshindi itajinyakulia kitita cha
shilingi laki moja pamoja na kombe litakaloandikwa jina la kata huku
mshindi wa pili akijinyakulia shilingi elfu hamsini.
"Mashindano
haya ni endelevu ambapo yatakuwa yakifanyika kila mwaka na watakuwa
wakishindania vikombe hivi ambavyo vinatolewa katika kila kata huku
katika ngazi ya tarafa na wilaya zikishindaniwa zawadi nyingine zaidi".
Alisema Kamonga.
Ameongeza kuwa timu zitakazoshinda kwa ngazi ya
tarafa na wilaya zitapewa zawadi kubwa zaidi kuliko zilizotolewa kwa
washindi wa ngazi ya kata.
Michuano ya ligi ya mbunge wilayni Ludewa mkoani Njombe ikiendelea katika kata mbalimbaliBaadhi ya wachezaji wa ligi ya mbunge wakiwaapunziko ligi kuanza tena
Awesome and interesting article. Great things you've always shared with us. Thanks. Just continue composing this type of post.
ReplyDelete