MISS ILALA KUPATIKANA JULAI 31, "TUNAMPONGEZA RAIS KUMTEUA BASILA KUWA DC - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 25, 2021

MISS ILALA KUPATIKANA JULAI 31, "TUNAMPONGEZA RAIS KUMTEUA BASILA KUWA DC

 

Warembo wakiwa pamoja na Kamati nzima ya Miss ilala kwa Mwaka huu wa 2021, ambapo wamefanikiwa kuingia warembo 17 na kutokana na Hali ya uchumi kwa Mwaka huu hawatakaa kambini
Muandaaji wa shindano la Miss ilala Lucas Rutainiwa akiwa Miss ilala 2018 Linda peter pamoja na Mmiliki wa Hoteli ya Onomo ambao ni moja ya wadhamini wa shindano hilo sanjari na baadhi ya Warembo waliofanikiwa kupita Kwenye usaili.


*****************************

Khadija: Khadija Seif, Michuzi TV

MASHINDANO ya kumpata Malkia wa Urembo Wilaya ya Ilala 'Miss Ilala' yamezinduliwa rasmi leo ambapo yanatarajiwa kufanyika Julai 31 mwaka huu.

Akizungumza na wandishi wa habari mapema leo, muandaaji wa shindano hilo la urembo, Lucas Rutainiwa, amesema kuwa mashindano yameanza rasmi kwa kuwa washamaliza usaili wa kuwapata washiriki wa shindano hilo.

"Warembo watakuwa wanakuja mazoezini na kurudi nyumbani hawatakaa kambini hadi siku ya finali na baada ya finali Julai 31 washindi watatu wataenda kuwakilisha ngazi ya Miss Tanzania na tulifanikiwa kupata warembo 17 kwenye usaili."

Washindi hao watakutana na warembo wa Tanzania nzima wakiwemo na wa mikoani na kupatikana mrembo mmoja atakaye iwakilisha Nchi kimataifa katika ngazi ya Dunia Miss World" Amesema Rutainiwa.

Rutainiwa pia amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua muandaaji wa Miss Tanzania, Basila Mwanukuzi kuwa Mkuu wa Wilaya huku akimtaka Basila kufanya kazi kwa bidii na uaminifu ili alinde Imani ya Rais aliyoiweka kwake.

" Kitendo cha Rais Samia kumteua Basila kuwa Mkuu wa Wilaya kinatoa picha ya namna gani tasnia ya Urembo imepiga hatua na inaheshimiwa, ni wajibu wetu tulio katika kiwanda hiki cha Urembo kuilinda Imani hiyo ya Rais wetu," Amesema Rutainiwa.

[11:39, 24/06/2021] Khadija: Muandaaji wa shindano la Miss ilala Lucas Rutainiwa akiwa Miss ilala 2018 Linda peter pamoja na Mmiliki wa Hoteli ya Onomo ambao ni moja ya wadhamini wa shindano Hilo sanjari na baadhi ya Warembo waliofanikiwa kupita Kwenye usaili

[11:39, 24/06/2021] Khadija: Warembo wakiwa pamoja na Kamati nzima ya Miss ilala kwa Mwaka huu ambapo wamefanikiwa kuingia warembo 17 na kutokana na Hali ya uchumi kwa Mwaka huu hawatakaa kambini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad