HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 9, 2021

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AZUNGUMZA NA RAIS NDAYISHIMIYE WA BURUNDI

Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango Ofisini kwake Ikulu Gitega Burundi kwa ajili ya Mazungumzo. Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amemuwakilisha Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana katika Mji Mkuu wa Serikali Gitega Nchini Burundi.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu Gitega Nchini wakati Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amemuwakilisha Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana katika Mji Mkuu wa Serikali Gitega Nchini Burundi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango, akiagana na Baadhi ya Watumishi wa Taasisi za Serikali ya Burundi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melkior Ndadaye Bujumbura Burundi, alipokuwa akirejea Nchini Baada ya kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye kumbukizi ya kutimiza Mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza iliyofanyika jana katika Mji Mkuu wa Serikali Gitega Nchini Burundi.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad