Na Munir Shemweta, WANMM MVOMERO
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameagiza kufanyika upekuzi wa
mashamba 86 yasiyoendelezwa katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ili
yatakayobainika kutoendelezwa, mapendekezo ya kufutwa yapelekwe kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani.
Waziri
Lukuvi alitoa agizo hilo leo tarehe 8 Juni 2021 wakati akizungumza kwa
nyakati tofauti na viongozi, watendaji wa kata za wilaya ya Mvomero na
wananchi wa Wami Dakawa akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani
Morogoro.
Alisema,
katika wilaya ya Mvomero kuna mashamba 86 ambayo uendelezaji wake una
mashaka hivyo ni vizuri ukafanyika upekuzi haraka na yale yasiyokidhi
vigezo wamiliki wake wapewe notisi za ufutaji na kusisitiza kuwa
serikali haitaacha kuchukua hatua kwa mashamba yasiyoendelezwa.
"
Ningefurahi katika kipindi cha miezi miwili ya sita na saba 2021 kazi
ya upekuzi mashamba hayo iwe imefanyika ili kupunguza migogoro ya ardhi
kati ya wamiliki na wananchi na lazima hatua zichukuliwe" alisema
Lukuvi.
Kwa
mujibu wa Lukuvi, kazi ya upekuzi mashamba ni ya msingi na waliopewa
mashamba wafahamu kuwa walipewa mashamba ili kuyaendeleza na sheria
inataka mmiliki wake walau awe ameendeleza moja ya nane ya shamba zima
kwa mwaka mmoja.
"Tatizo
la Mvomero ardhi imechukuliwa na wamiliki wake wamefungia hati bila
kulipa kodi wala kuendelezwa na upekuzi huu unaofanyika ni kutaka kujua
kila halj ya shamba" alisema Lukuvi
Naye
Mbunge wa Jimbo la Mvomero Jonas Van-zeland alisema, wilaya Mvomero
inayo migogoro mingi ya ardhi ikiwemo utelekezaji mashamba jambo
alilolieleza kuwa limechangia wananchi kushindwa kufanya shughuli za
kijamii na kuongeza kuwa wamiliki wa mashamba hayo wengi hawajulikani na
wananchi.
Aidha,
Waziri Lukuvi katika ziara yake wilayani Mvomero alisema, wilaya hiyo
imekuwa na migogoro mingi ya ardhi ikiwemo ile ya mipaka ya vijiji na
wilaya na kubainisha kuwa jukumu la kutafuta suluhu ya migogoro ya
mipaka ni la viongozi wa mkoa na wilaya.
"
Why migogoro ya mipaka inaendelea wakati wilaya na mkoa ipo na mipaka
iliyopo ni ya kiutawala na isiwe kikwazo cha shughuli za wananchi na mtu
asizuiwe kuchunga nje ya mipaka ya kiutawala cha msingi pawepo
utaratibu" Waziri Lukuvi.
Katika
hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Sukuhu Hassan ameendelea kushusha neema kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro
ambapo safari hii amefuta jumla ya mashamba 9 yenye ukubwa wa ekari
13,900.5 katika halmashauri ya wilaya ya Mvomero na kuelekeza sehemu
kubwa ya mashamba itumike kutatua shida za wananchi.
Waziri
Lukuvi alisema kati ya ekari zilizofutwa ekari 9,700 zigawiwe kwa
wananchi kwa ajili ya matumizi mbalimbali na ekari 4,100 zitengwe kwa
ajili ya shughuli za uwejezaji na kusisitiza watakaopewa hawatakiwi
kuyauza.
"
Rais amesisitiza kila eneo lililofutwa basi kipaumbele kiwe kwa
wananchi ambao hawana ardhi hasa vijana wasiowahi kuwa na ardhi ama
zile kaya zisizomiliki ardhi" alisema Lukuvi.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Martine Shighela kwa upande wake mbali na
kumshukuru Lukuvi kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha miaka
mitano katika sekta ya ardhi ameweka wazi kuwa utatuzi wa migogoro ya
ardhi anaoufanywa na Waziri Lukuvi haulengi mtu mmoja mmoja bali
unawalenga walio wengi na kusema kuwa huo ni utekelezaji wa sera ya
Chama cha Mapinduzi.
Ametaka
kuwepo ushirikiano kati ya uongozi wa mkoa na wananchi wa Mvomero
katika kutekeleza maekekezo ya serikali na kutafuta ufumbuzi wa matatizo
mengine yasiyohusiana na sekta ya ardhi.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza
Viongozi, Madiwani na Watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mvomero
katika ukumbi wa halmashauri mkoani Morogoro tarehe 8 Juni 2021.
Mbunge
wa Jimbo la Mvomero Jonas Van-Zeland akizungumza mbele ya wananchi wa
Wami Dakawa katika halmashauri ya wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro
wakati wa ziara ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
William Lukuvi tarehe 8 Juni 2021.
ananchi
wa Wami Dakawa wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro wakimsikiliza Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ( hayupo pichani )
wakati wa ziara ya kilazi katika mkoa wa Morogoro tarehe 8 Juni 2021.
No comments:
Post a Comment