Miongoni mwa zawadi zilizotolewa na Kampuni ya Fimbo cycle katika siku ya watoto (Asas mtoto day out iliyoandaliwa na Mwanadada Dina Marious
Na.Khadija Seif, Michuziblog
WANAWAKE Watakiwa kuiga Mfano mzuri wa Dina Marious katika kuiweka karibu jamii hasa watoto katika Sekta ya Michezo na Kimasomo.
Akizungumza na Michuzi Tv Meneja Masoko wa Kampuni ya Fimbo cycle Modric Hussein, ambayo Kampuni hiyo ni mojawapo ya wadhamini katika hafla ya watoto (Asas Mtoto day Out) iliyoandaliwa na Mtangazaji wa kipindi Cha uhondo kutoka Efm nchini amesema wakati Mwengine watoto wanahitaji kujumuika pamoja na kufurahi ili waweze kujifunza vingi kimasomo pamoja na Kimichezo.
"Hafla hii ya "Asas Mtoto day Out" Ina vingi Sana na inawajengea watoto ujasiri kupitia Mashindano mbalimbali yanayofanyika katika siku hiyo hasa Michezo ambapo unakuta watoto wengi hushiriki na kutaka kushinda hivyo kwa namna moja au nyingine inamjengea mtoto uwezo wa kuwa jasiri na mchangamfu."
Hata hivyo Meneja huyo ameeleza msukumo wake wa kutaka Kudhamini hafla hiyo huku akitaja Dina Marious kuwa mfano wa Mwanamke wa kuigwa katika jamii yetu.
"Ni kwa Mara ya kwanza tumeonelea Kushirikiana na Dada Dina kutoa zawadi kwa watoto wetu hasa walioibuka washindi kupitia Michezo katika jukwaa na tumetoa Baiskeli 5 na tunategemea mwakani kuendelea kutoa udhamini huu na zaidi ya Baiskeli hizi ."
Pia amesema Kampuni hiyo inajushugulisha na bidhaa za usafiri,Chupa za maji pamoja vingine vingi.
No comments:
Post a Comment