Mkufunzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bibi. Mwadawa Twalibu Nchemwa akiwasilisha mada kuhusu maadili ya utumishi wa umma wakati wa mafunzo hayo kwa watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) jana jijini Dodoma.Mkufunzi kutoka Tume ya Utumishi wa Umma, Bibi. Pricila Ambelile akiwasilisha mada kuhusu haki na wajibu wa mtumishi wa umma wakati wa mafunzo kwa wafanyakazi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) kuhusu masuala mbalimbali ya utumishi wa umma ikiwemo namna ya ujazaji wa OPRAS, Sheria ya Utumishi wa Umma na Haki na wajibu wa mtumishi wa umma.Mmoja wa watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa vya Siasa(ORPP) akichangia mada wakati wa majadiliano kuhusu muongozo wa aina ya mavazi yanayofaa kwa watumishi wa ummawanaume wakati wa mafunzo kuhusu maadili ya watumishi wa umma kwa wafanyakazi wa Ofisi hiyo jana jijini Dodoma. Baadhi ya wafanyakazi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) wakifuatilia mada wakati wa mafunzo kwa wafanyakazi hao kuhusu masuala mbalimbali ya utumishi wa umma ikiwemo namna ya ujazaji wa OPRAS, Sheria ya Utumishi wa Umma, maadili ya mtumishi wa ummana na namna ya kushughulikia malalamiko.
Watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa(ORPP) wakila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu katika Utumishi wa Umma mara baada ya kupata mafunzo kuhusu madaadidli ya watumishi wa umma yaliyotolewa jana jijini Dodoma. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wapo katika mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uelewa katika masuala mbalimbali ya utumishi wa umma. (Picha na ORPP)
No comments:
Post a Comment