WASHINDI wa Uni talent wakabidhiwa zawadi zao huku wakisisitizwa kuendeleza vipaji hivyo ili kujikwamua kiuchumi .
Akizungumza na Waandishi Wahabari Mara baada ya kukabidhi zawadi hizo Afisa Mwandamizi wa Baraza la Sanaa (BASATA) Abel Ndaga amesema Baraza halitosita kutoa vibali na kushiriki kikamilifu kwa Wadau wenye lengo la kuibua na kukuza vipaji.
"Huu ni Msimu wa pili lakini bado lengo ni lile lile hivyo Baraza limeona mnania ya dhati kukuza vipaji vya vijana hivyo hatutosita kukuza vipaji hivyo tukiwa kama walezi wa Sanaa nchini."
Pia amesema ana matumaini makubwa kwa Msimu ujao wa Shindano na kuwataka vijana kukimbilia fursa hiyo.
Washindi ambao wamepatikana kwenye Shindano hilo ni washindi watatu walipatikana waliokidhi vigezo na kupitia mchujo kwa majaji hao na Miongoni mwa majaji ni Gnako kutoka kundi la weusi.
Mshindi wa Kwanza ni kikundi cha watu wanne ambao ni muungaiko kutoka vyuo tofauti ikiwemo Muhimbili, t.i.a,Udsm pmaoja chuo Cha Ardhi.
Washindi hao wamekabidhiwa hundi ya Shilingi milioni 10,huku Mshindi wa pili akilamba milioni 3 na wa mwisho milioni 1.
Kwa upande wake Mshindi wa pili aliyejulikana kama tiga amesema Mashindano yalikua ni ya haki na anashukuru Kampuni ya Maroon entertainment kwa kueza kuona fursa ya vijana hasa wanachuo kuonyesha vipaji vyao .
"Ni Jambo la kupongeza wadau wanaondelea kukuza vipaji vya vijana kwa namna moja au nyingine wanasaidia vijana kuondokana na vitendo viovu pamoja na kujisaidia wenye hasa kwenye ajira."
Hata hivyo Mshindi huyo amesema fedha alizozipata anaenda kukamilisha mpango wake wa kujenga kaburi la Mama yake Mzazi.
"Ahadi yangu imekamilisha na Shindano la Uni talent nawapongeza na nashukuru Sana kwa nafsi niliyoipata na nahaidi kukiendeleza kipaji changu."
No comments:
Post a Comment