Waziri
wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile
akisisitiza jambo kwa washiriki wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) ikiwasilisha taarifa kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti kwa
Wabunge. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundombinu Mhe. Seleman Kakoso kilichofanyika leo Mei 17,2021 bungeni
jijini Dodoma.
Waziri
wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile
akizungumza wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikitoa semina
kwa wabunge kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti Kulia ni Naibu
Spika wa Bunge. Dkt. Tulia Ackson na katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Seleman Kakoso ,Semina hiyo
imefanyika leo Mei 17,2021 bungeni jijini Dodoma.
Naibu
Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akifunga kikao cha Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania baada ya kuwasilisha taarifa kuhusu huduma za
mawasiliano na intaneti kwa Wabunge. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile na katikati ni Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Seleman Kakoso
kilichofanyika leo Mei 17,2021 bungeni jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Kuwe
akiwasilisha taarifa kuhusu huduma za mawasiliano na intaneti kwa
Wabunge kwa niaba ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.
Faustine Ndugulile iliyofanyika leo Mei 17,2021 bungeni jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab
Chaula (kushoto) akifuatilia wasilisho la Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Kuwe (hayupo pichani) kuhusu
huduma za mawasiliano na intaneti kwa Wabunge .Anayefuata ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Tathmini na Ufuatiliaji wa Wizara hiyo, Elisa Mbise
kilichofanyika leo Mei 17,2021 bungeni jijini Dodoma.
Baadhi
ya Wabunge wakifuatilia wasilisho la Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabri Kuwe (hayupo pichani) kuhusu
huduma za mawasiliano na intaneti kwa Wabunge kwa niaba ya Waziri wa
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile
kilichofanyika leo Mei 17,2021 bungeni jijini Dodoma.
………………………………………………………….
Waziri
wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Faustine Ndugulile amesema
kuwa Wizara yake iko mbioni kupeleka Bungeni muswada utakaowezesha
kutungwa kwa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi iili kulinda faragha na
taarifa za mwananchi
Kauli hiyo ameitoa leo Mei 17,2021 bungeni
jijini Dodoma wakati wa Semina kwa wabunge yenye lengo la kujua huduma
za mawasiliano na intaneti ili waweze kufahamu namna Wizara
inavyotekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini
yake
Dkt.Ndugulile amesema kuwa tayari wizara imeshaandaa sheria
hiyo ili kulinda faragha na taarifa binafsi za wananchi katika hatua ya
ukusanyaji wa taarifa, usafirishaji, matumizi na utunzaji wa taarifa
hizo.
Hata hivyo amewataka Wabunge kuwa tayari pindi pendekezo
la muswada litakapowasilishwa Bungeni ili sheria hiyo iweze kutungwa kwa
maslahi mapana ya taifa
“Mkiangalia kwa sasa uharamia na
ujambazi umehama kutoka silaha za mkononi na kuhamia mtandaoni, Serikali
itaendelea kuelimisha wananchi, kuboresha mifumo na teknolojia ili nchi
iwe mbele zaidi katika kudhibiti uhalifu mtandaoni,” amesema Dkt.
Ndugulile
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Kuwe amesema kuwa nchi inaelekea kutumia
huduma ya 5G na majaribio yatafanyika ili kuhakikisha kasi ya teknolojia
inayotakiwa inapatikana ili kuongeza huduma ya mawasiliano ya data
nchini
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundombinu, Seleman Kakoso ameishauri Serikali kuongeza fedha za
kuuwezesha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutoa ruzuku ya kutosha
kwa kampuni za simu ili mawasiliano yafike kwa wananchi wote pamoja na
kuongeza usikivu wa redio kwenye maeneo ya mipakani
Naye Naibu
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Akson ametoa pongezi kwa Wizara kwa kuleta
semina hiyo kwa Wabunge na anatamani katika kipindi kifupi Wabunge
wasizungumzie changamoto ya mawasiliano katika maeneo yao kwa kuwa
mawasiliano ni huduma ya msingi kama ilivyo maji, barabara
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
No comments:
Post a Comment