Benki ya Equity (T) wiki hii imezindua rasmi kampeni ya “Mara tatu zaidi na Jijenge Akaunti” jijini Mwanza na kuwa gumzo kubwa kwa wananchi wa jiji hilo.
Promosheni hii imekuwa gumzo jijini humo baada ya wafanyakazi wa Benki hiyo kuingia katika mitaa ya jiji la Mwanza na kuwafungulia akaunti wateja katika maeneo yao ya kazi na biashara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni za “Pata Mara tatu Zaidi na Jijenge ya Equity Bank” kwenye mitaa karibu na viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Equity (T), Godwin Semunyu amesema “Equity Bank inaamini katika uwezeshaji wa wateja wetu na wanachi wote kwa ujumla ndio maana tukabuni akaunti hii ya Jijenge ambayo inaruhusu wateja kujiwekea akiba kidogo kidogo na hatimaye kuweza kuchukua mkopo wa zaidi ya mara tatu wa akiba atayoukuwa amajiwekea kwa kipoindi cha miezi sita na kuendelea”.
Zaidi ya kupata mkopo wa mara tatu wa kaisi alichijiwekea, akaunti ya Jijjenge pia inawapa fursa wateja kupata riba shindani huku kukiwa hakuna kabisa makato ya uemdeshaji. Ni akaunti uya kwanza nchini kutoa wigo mkubwa Zaidi wa ukopeshaji.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Equity Bank (T) Godwin Semunyu akisalimiana na mteja wakati wa halfla ya wateja wa Benki hiyo jijini Mwanza.
Akizungumza kuhusu promoshieni hiyo mkazi wa Nyegezi Jijini Mwanza Bi.Aisha Salmin alisema “Nimeipenda sana huduma na promosheni hii sababu imekuja kutupa ahueni sisi wafanyabishara wadogo ambao tumekuwa wagumu kukopesheka kwa kukosa dhamana, kwani kupitia Jijenge Akaunti ya Equity Bank pesa zetu wenyewe sasa zitatudhamini ili kupata mikopo. Nawashukuru sana Equity Bank”.
No comments:
Post a Comment