Ecobank Tanzania imeendelea na kampeni ya kuingia mtaani ya kutangaza huduma na kazi zinazotolewa na Benki hiyo katika Mkoa wa Mwanza pamoja na mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa, May 28 hadi 30, 2021.
Benki hiyo imejikita kutoa Elimu kwa wateja wao wa ambao ni Wafanyabiashara wa Kati, wa wadogo na wakubwa pamoja na wale ambao sio wateja wao kuhusu huduma za Kibanki zinazotolewa na Benki hiyo ili kuweza kupanua wigo wa ufahamu hasa kwenye kutunza akiba, huduma zitakazitolewa ni pamoja na elimu ya Mkopaji na jinsi ya kupata mkopo kwa riba nafuu.
Elimu hiyo pia imetolewa kwa Wafanyabiashara hao kuhusu Akaunti za Benki hiyo ambazo ni (Current Account, Savings Account, Express Account, Termed Diposit Account).
Ecobank Tanzania inaendelea kuunga mkono mikakati ya Serikali ya kuongeza tija katika sekta ya huduma za fedha na kupanua huduma hizo ili kuwafikia watanzania walio wengi na ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki.
Pia Benki hiyo imetoa shukrani kwa wananchi waliotoa muda wao kusikiliza huduma
No comments:
Post a Comment