Amesema Benki ya Tanzania, inajivunia ubunifu ambao kwao ni kipaumbele na wataendelea kutengeneza huduma na bidhaa ambazo zitaweza kumudu uwezo wa kila mwananchi na wafanyabiashara na kwa kiwango kinachoridhisha.
Aidha amesema kuwa wataendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuhakikisha miundombinu inaendelea kuboreka.
"Equity Bank tunasimamia dira na miongozo kwa kusikiliza na kujali wateja na huo ndio msimamo na utekelezaji wa benki yetu kwa wananchi." Amesema.
Akizugumza baada ya kukabidhi mfano wa hundi hiyo kwa Mheshimiwa Waziri Chamuhiro, Mkuu wa Masoko wa Benki ya Equity Godwin Semunyu amesema kuwa Benki ya Equity ni mdau mkubwa wa sekta ya ujenzi nchini hivyo imeona umuhimu wa kudhamini mkutano huo ili kuwakutanisha wadau wote wa sekta hiyo kwa lengo la kubadilishana uzoefu na hivyo kuongeza tija.
“Equity Bank
imejipanga kuendelea kutoa huduma nafuu za kifedha kwa wakandarasi wa ndani ili kuwaongezea mitaji na hivyo kuwapa uwezo wa kushindana sokoni.
Nichukue fursa hii kuwakaribisha wakandarasi wote nchini kutembelea matawi yetu
ya Benki ya Equity ili wafurahie huduma bora na nafuu zaidi sokoni” alisema.
Benki ya Equity pia imeandaa sehemu maalum katika jengo la Daimond Jubilee ambapo mkutano huo unafanyika, ili kutoa maelezo ya bidhaa zake kwa washiriki wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment