Waziri wa 
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo 
amesema Serikali kwa kushirikiana na mamlaka husika itaandaa Mkakati wa 
udhibiti wa athari za zebaki kwa afya ya binadamu na mazingira.
Jafo
 amesema hayo leo Aprili 27 wakati akiwasilisha Hotuba ya Mapato na   
Matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 bungeni jijini Dodoma.
Alisema
 sambamba na hayo itaainisha na kufanya tathmini ya maeneo yenye 
shughuli nyingi za uchimbaji mdogo wa dhahabu kwa kutumia zebaki na 
kuweka mikakati ya kuyarejesha katika hali yake ya asili.
Aidha, 
waziri huyo aliongeza kuwa katika kutekeleza Mpango-kazi wa Taifa wa 
kupunguza matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu nchini 
Serikali itatoa mafunzo kwa mamlaka zinazohusika na udhibiti wa zebaki 
kuhusu namna ya kudhibiti uingizaji, matumizi na utupaji wa taka 
zitokanazo na zebaki nchini. 
Katika hotuba hiyo pia alisisitiza 
kuwa Serikali itaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala kwa 
kuandaa Mkakati wa Nishati Mbadala ya Kuni na Mkaa kwa ajili ya kupikia 
na kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi ya nishati mbadala.
“Mheshimiwa
 Spika tutaendelea kutoa elimu ya nishati mbadala hususan hususan kwa 
taasisi zinazotumia kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia zikiwemo magereza,
 polisi, na taasisi za elimu. Katika kipindi hiki, Ofisi itaendelea na 
ufuatiliaji wa utekelezaji wa mipango iliyowekwa na taasisi mbalimbali 
kuhusu matumizi ya nishati mbadala,” alisema.
Kwa upande wake 
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na 
Mazingira Mhe. Eric Shigongo alishauri Ofisi ya Makamu wa Rais 
ishirikiane na Ofisi ya Mkemia Mkuu kudhibiti uingizwaji wa zebaki 
nchini.
Katika hotuba hiyo aliyoiwasilisha kwa niaba ya 
Mwenyekiti Mhe. David Kihenzile alishauri Serikali itafute teknolojia 
mbadala ambayo wachimbaji hao wataitumia ili kuachana na matumizi ya 
zebaki.
“Uingizaji holela na utumiaji wa kemikali ya Zebaki 
nchini kutokana na kuwapo kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu wanotumia 
kemikali hiyo, unaathiri kwa kiasi kikubwa afya na usatwi wa wchimbaji 
hao. Madhara ya matumizi ya kemikali hiyo yanatokana na wachimbaji wengi
 kuitumia bila ya kuwa nyenzo za kujinga kutokana na zebaki,” alisema.
Shigongo
 ambaye pia ni Mbunge wa Buchosa alitahadharisha kuwa maji yanayotumika 
kusafishia dhahabu yakiwa yamechanganyika na Zebaki, yanatiririkia 
kwenye vyanzo vya maji na kuwa watu wanapotumia maji hayo.
Naye 
Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Hawa Mchafu alishauri Serikali itumie fedha 
kutoka mifuko ya mazingira kwa kusaidia katika kujenga uelewa wa 
kupunguza matumizi ya zebaki.
Pia Mbunge huyo alipendekeza njia 
mbadala ya matumizi ya zebaki na kusema kuwa kemikali hiyo ina athari 
kubwa kwa binadamu hususan katika maeneo ya Kanda ya Ziwa ambako kuna 
shughuli za uchimbaji wa dhahabu.
6.6 Matumizi ya kemikali hatarishi – Zebaki 
Mheshimiwa
 Spika, uingizaji holela na utumiaji wa kemikali ya Zebaki nchini 
kutokana na kuwapo kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu wanotumia kemikali 
hiyo, unaathiri kwa kiasi kikubwa afya na usatwi wa wchimbaji hao. 
Madhara ya matumizi ya kemikali hiyo yanatokana na wachimbaji wengi 
kuitumia bila ya kuwa nyenzo za kujinga kutokana na zebaki. Vilevile, 
maji yanayotumika kusafishia dhahabu yakiwa yamechanganyika na Zebaki, 
yanatiririkia kwenye vyanzo vya maji kama vile mito na mawaziwa. Watu 
wanapotumia maji kutoka vyanzo hivyo vilivyochafuliwa na zebaki ya 
kuoshea dhahabu, huathirika kiafya na wakati mwingine kupata maradhi 
sugu yanayogharimu maisha yao. 
Mheshimiwa Spika, Kutokana na hali hiyo, Kamati inashauri kuwa:- 
i) Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira ishirikiane na Ofisi ya Mkemia Mkuu kudhibiti uingizwaji na zebaki nchini; 
ii) usimamizi na uratibu matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu nchini 
25 
uendelezwe na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa pamoja na Ofisi ya Mkemia Mkuu; na 
iii) Serikali itafute teknolojia mbadala ambayo wachimbaji hao wataitumia ili kuachana na matumizi ya zebaki. 
6.7 Taarifa ya Hali ya Mazingira nchini 
Mheshimiwa
 Spika, Kifungu 175 (1) cha Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 kinamtaka 
Mkurugenzi wa Mazingira kuandaa na kutoa taarifa juu ya Hali ya 
Mazingira nchini kila baada ya miaka 2 na kuiwasilisha Bungeni. Hata 
hivyo uzoefu unaonesha kuwa upo ugumu wa kutekeleza masharti hayo jambo 
lililosababisha kuwasilishwa kwa taarifa hiyo mwaka 2008, 2014 na 2019. 
Kwa sababu hiyo, taarifa ya kwanza, ya pila na ya tatu hazikuweza 
kuzingatia masharti ya kuwasilishwa baada ya miaka miwili. Kwa msingi 
huo, Kamati inashauri kuwa Serikali iandae mapendekezo ya marekebisho ya
 kifungu hicho kwa kuongeza muda wa kutoa ripoti kufikia miaka 5.
Tuesday, April 27, 2021
 
Home
HABARI
Waziri Jafo awasilisha Hotuba ya Mapato na   Matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 bungeni jijini Dodoma
Waziri Jafo awasilisha Hotuba ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 bungeni jijini Dodoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
 

 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment