WAZIRI AWESO AIPONGEZA EQUIT BANK (T) KWA KUCHANGIA MAENDELEO YA MAJI NCHINI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 18 April 2021

WAZIRI AWESO AIPONGEZA EQUIT BANK (T) KWA KUCHANGIA MAENDELEO YA MAJI NCHINI

 Waziri wa Maji, Juma Aweso akishuhudia wakati Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Equity (T), Esther Kitoka akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Dodoma, Aron Joseph Augustine mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji katika shule ya msingi Makole Dodoma

------------

Waziri wa Maji Juma Aweso ameipongeza Benki ya Equity kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa maji nchini na kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) ili kuchangia uwekwaji wa miundombinu ya maji katika shule msingi Makole, Dodoma. 

Waziri  Aweso alisema hayo wakati wa hafla ya uzunduzi wa kampeni ya kitaifa  ya kupambana na upotevu wa maji nchini uliofanyika katika ukumbi wa Mtakatifu Gaspar jijini Dodoma.
Akiongea kabla ya kukabidhi  hundi hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Equity-Tanzania Bi. Esther Kitoka alisema kuwa  kwa kipindi kirefu sasa Benki ya Equity imekuwa mdau mkubwa wa maji hapa nchini kupitia uwezeshaji kwa wananchi na taasisi.

“Wote tunafahamu kuwa maji ni uhai na kuwa bila maji, hakuna shughuli zozote za uzalishaji zinaweza kufanyika. Benki ya Equity ikiwa kama mdau mkubwa katika sekta ya maji nchini, leo tunatoa mchango wa shilingi milioni Kumi ili kuweka maji na mioundombinu ya maji-taka katika shule ya Msingi Makole hapa Dodoma. Msaada huu unalenga kuboresha hali ya afya na usafi kwa Watoto wetu wa shule ya  Makole na maeneo ya jirani” alisema Bi.Kitoka.
 
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Equity,  Esther Kitoka akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kudhibiti upotevu wa maji nchini.

Akielezea zaidi kuhusu ushiriki wa Benki ya Equity katika harakati za kuondoa changamoto za upatikanaji wa maji nchini, Bi Kitoka alisema “Benki ya Equity imekuwa ikishiriki kikamilifu kwa kutoa huduma za kifedha na zisizo za kifedha katika kukabiliana na tatizo sugu la upotevu wa maji katika mzunguko mzima. Kuanzia kwa kuunganishwa maji mpaka uchimbwaji wa visima kwa watu binafsi, vikundi na hata taasisi. Mikopo yetu ya huduma za maji ijulikanayo kama “WASH” (Water Sanitation and Hygiene) ina lengo la kuongeza upatikanaji wa Maji Safi na  kuboreha Usafi wa Mazingira (maji taka)” alisema.

Akifanunua kuhusu mgawanyiko huo, Bi Kitoka alisema; “Huduma za WASH  zipo katika makundi mawili ambayo ni upatakanaji wa maji safi na usafi wa mazingira (maji taka). 
Katika mikopo ya kitengo cha upatikanaji wa maji safi na salama, Benki ya Equity  inakopesha maeneo yafuatayo:
Uboreshaji wa miundombinu ya maji
Maunganisho ya maji  kutoka kwenye bomba kuu
Ukopeshaji wa Matangi ya kuhifadhia maji (plastiki, saruji, chini ya ardhi)
Uchimbaji wa Visima vifupi
Ununuzii wa Pampu na vifaa vya maji 
Gharama za Maendeleo na ulinzi wa chemchemi za maji
Uchimbaji wa Mabwawa, na Visima virefu
Gharama za Mifumo ya usafishaji wa maji

Kwa upande wa mikopo ya Jamii Safi (Usafi wa Mazingira),  Benki ya Equity inalenga kukopesha katika mazingira yafuatayo:
Ujenzi na uboreshaji wa vifuniko
Ujenzi wa mashimo bora  ya maji taka
Kuunganisha kwa mifumo ya maji taka
Ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya usafi wa mazingira
Malori ya kukusanya taka / takataka
Huduma nyingine zitolewazo na Banki ya Equity kwenye sekta maji ni Pamoja na:
Mikopo kwa wakandarasi wa miradi ya maji ikiwemo (Letter of Credit na Asset financing)
Mikopo ya uendeshaji kwa mashirikokisjhi ya maji ya mikoa ili kuyaongezea ufanisi.
Equity Bank Tanzania Limited ni taasisi ya kifedha inayofanya kazi chini ya  Benki mama  ya Equity Group Holdings Plc iliyopo Kenya, Uganda, Sudan ya Kusini, Rwanda na DRC. Kwa sasa Benki ya Equity ina matawi 14, Mawakala  Wakuu zaidi ya 100 na Mawakala wadogo zaidi ya 3,600 nchi nzima. Benki  ya Equity pia hutoa huduma kupitia simu za mkononi na mtandao wa  intaneti.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad