WANANCHI WAIPONGEZA TCRA KWA KUSIMAMIA WATOA HUDUMA ZA SIMU ZA MKONONI KURUDISHA MABANDO YA AWALI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 16 April 2021

WANANCHI WAIPONGEZA TCRA KWA KUSIMAMIA WATOA HUDUMA ZA SIMU ZA MKONONI KURUDISHA MABANDO YA AWALI

 


Mkurugenzi wa TIBA, Marcela Lungu akizungumza faida ya kushuka kwa bando inavyotoa fursa katika uendeshaji wa Ofisi katika ununuzi wa vifurushi vya Internet.
Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) Hamisi Mchuchuri akizungumza faida ya kushuka kwa bando kurejea Awali kuwa kunapunguza gharama za maisha kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Mjasirimali wa Biashara ya Matunda Walter Hiristo akizungumza kuhusiana watoa huduma kuboresha huduma ya bando na kuipongeza TCRA kwa udhibiti.
Mfanyabiashara bidhaa kwa njia ya mtandao Clemance Mtembela akizungumzia bei ya bando kuwa chini.


*Wadai maisha yatakuwa rahisi katika kufanya biashara mtandaoni 

KUFUATIA hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Hassan Suluhu ya aliyoitoa katika uapishashaji wa Mawaziri na Kuitaka  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia upya  vifurushi vya Bando, TCRA imetekeleza hilo  kwa kuwataka  watoa huduma za kampuni za simu  kurudisha  vifurushi vya Bando kuwa vya bei isiyomuumiza mwananchi jambo ambalo limefanyika na kufanya wananchi kufurahia huduma hiyo.

Baada ya vifurushi kurejea na kufanya wananchi kuwa na uhakika wa kupata taarifa kwa njia ya mtandao pamoja na biashara kuendelea kufanyika kwa njia ya mtandao wananchi wametoa maoni tofauti na  kuipongeza Mamlaka hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti watumiaji wa vifurushi vya Bando la Internet wamesema kuwa maisha yalikuwa magumu kwao na huku baadhi wakishindwa kuendesha biashara kwa kutumia mtandao.

Mwanafunzi wa Chuo Cha Usafirishaji ( NIT) mwaka wa tatu Hamisi Mchuchuri amesema kuwa, bando kuwa juu lilikuwa linawaathiri katika masomo kutokana maisha ya Chuo kuwa ya bajeti.

Amesema kuwa kuna vitabu vingine viko mtandaoni hivyo bila kuwa fedha zaidi ya 5000 huwezi kupata lakini sasa unapata hata sh.1000 na 2000 na kupata vifurushi vya kuweza kupakua vitabu vyote.

Mchuchuri amesema TCRA kupitia watoa huduma za simu wameweza kuboresha huduma za bando.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhamamasishaji wa Wanawake kutumia mitandao (TIBA) Marcela Lungu amesema kuwa kama wanaasasi walikuwa wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya bando lakini sasa itapungua na kuweza kuwafikia wananchi kwa wakati.

Amesema wakati Ugonjwa wa Corona sehemu kubwa wanatumia mitandao kwa kununua bando kuendesha mikutano.

Kwa upande wa Mjasirimali wa matunda Walter Hirispo  amesema, maisha ya bando kuwa juu yanaathiri watu wote hasa wenye kipato cha kuwaida kushindwa kumudu maisha hayo.

Naye Clemance Mtembela mfanyabiashara wa Duka Mtandao amesema kuwa, biashara ya bando kurejea katika hali ya awali kumerahisha maisha kwa kuweza kuwafikia wateja wote kwa wakati na wakawa hewani.

Amesema  vifurushi vilivyokuwa juu baadhi ya watu walikuwa hawaingii mtandaoni kufanya biashara na hata wakiingia hawawezi kupakua huduma ndani ya mtandao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad