Prof. Mark Mwandosya alipokuwa Hospitalini, Nairobi, Kenya |
Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya uhai, zawadi ya Pasaka. Nawashukuru pia mke wangu Lucy Akiiki, watoto na wajukuu, familia za Kahigwa na ya Mwandosya, Madaktari na Wauguzi wangu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, na Hospitali ya Nairobi (Nairobi Hospital), AMREF Flying Doctors, Uongozi wa Stanbic Bank Tanzania Limited na Stanbic Kenya Ltd, Balozi Chirau Mwakewere na Mama Rose Mwakwere wa Nairobi, Mheshimiwa Jaji Paul Mugamba wa Mahakama ya Juu Uganda na Mama Grace Mugamba, familia ya Kabange wa Nairobi, na ndugu na marafiki wote wanaoendelea kunitakia heri na afya njema. Asanteni sana.
Huu ni ushuhuda wangu kwamba Corona/Covid 19 ipo Tanzania .
Prof. Mark Mwandosya akiwa eneo la Kilimani baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitalini, Nairobi, Kenya |
Maombi yangu kwa Mwenyezi Mungu ni kwamba, ikiwezekana, Mtanzania mwingine awaye yote aepushwe na mateso na taabu za kukabiliana na maradhi haya. Hakika siwezi kumtakia mtu mwingine yeyote, hata aliye adui yangu mkubwa namna gani, kama yupo, apate ugonjwa huu.
Tutakiane Pasaka njema. Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania.
Pro Deo et patria.
No comments:
Post a Comment