HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 24, 2021

RAS MOROGORO: HALMASHAURI ZOTE ZA MKOA WA MOROGORO TUMIENI WATAALAM WANAOZALISHWA NA CHUO

Mgeni Rasmi, Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emanuel Kalobelo.

Na Mwandishi Wetu

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro amezitaka halmashauri zote za mkoa wa Morogoro kuanza kutumia wataalamu wanaozalishwa na chuo cha Ardhi Morogoro ili kutatua migogoro ya ardhi.

Kaui hiyo imetolewa na Mhandisi Emanuel Kalobelo alipokuwa Mgeni rasmi katika Mahafali ya 39 ya Chuo cha Ardhi Morogoro. 

Akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhandisi Kalobelo ameongeza kwamba ni aibu kwa Mkoa wa Morogoro kuwa na migogoro mingi ya Ardhi ilihali chuo kinachozalisha wataalamu wa upimaji na mipango miji kipo Mkoani humo. 

Nae Mkuu wa Chuo Bw Huruma Lugalla katika hotuba yake amesema, Chuo kitaendelea kutoa elimu bora ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi, vifaa vya upimaji, uchoraji pamoja na vifaa vya TEHAMA ili wanafunzi waendane na kasi ya teknolojia. 

Mahafali hayo yalitanguliwa na Kikao cha Bodi kilichokaa siku moja kabla, ambapo Mwenyekiti wa Bodi Profesa Mpanduji alipongeza uongozi wa chuo kwa kuchukua hatua na kuongeza kasi ya upimaji baada ya kupata ripoti ya kupima viwanja zaidi ya 19,000 ndani ya miezi miwili. 

Jumla ya wanafunzi 394 wamehitimu katika kozi za Jiomatikia (Upimaji Ardhi) na Mipango miji, katika ngazi za Astashahada ya awali, Astashahada na Stashahada.
Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emanuel Kalobelo akisaini kitabu cha wageni alipofika Chuo cha Ardhi Morogoro.
Mgeni Rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emanuel Kalobelo (wa pili toka kushoto) akipata maelekezo ya kifaa cha upimaji (total station) kutoka kwa mmoja wa wanafunzi. Upande wa Mgeni Rasmi yupo Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Morogoro na upande wa Kushoto yupo Mkuu wa Chuo
Brass band wakiongoza maandamano ya Mgeni Rasmi kuingia ukumbini
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi pamoja na baadhi ya wahitimu katika chuo hicho

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad