Kitengo cha Wateja Binafsi cha Ecobank Tanzania kikiongozwa na Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi, Salma Mkambara imetembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutoa elimu kwa Waheshimwa wabunge na wafanyakazi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu huduma za Kibanki zinazotolewa na Benki hiyo.
Ecobank Tanzania inaendelea kuunga mkono mikakati ya Serikali ya kuongeza tija katika sekta ya huduma za fedha na kupanua huduma hizo ili kuwafikia watanzania walio wengi na ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki.
Mkuu
wa kitengo cha Wateja binafsi kutoka Ecobank Tanzania, Salma
Mkambara(kushoto) akizungumza na Spika wa Bunge la Tanzania,
Job Ndugai(wa pili kushoto) pamoja na mbunge mwingine kuhusu namna Benko
hiyo ilivyojipanga kuwafikia watu wengi hapa nchini wakiwemo wabunge.
Wa pili kulia ni Meneja Mahusiano wa wateja Maalum kutoka Ecobank
Tanzania Jackline Nyangoe
Mkuu
wa kitengo cha Wateja binafsi kutoka Ecobank Tanzania, Salma Mkambara
pamoja na Meneja Mahusiano wa wateja Maalum kutoka Ecobank Tanzania
Jackline Nyangoe wakimsikiliza Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai
aliokuwa anauliza maswali kuhusu huduma zitolewazo na Benki hiyo wakati
wa kutoa elimu kwa wabunge na wafanyakazi wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akisoma moja ya vipeperushi vya Ecobank Tanzania alipotembelea banda la benki hiyo kwa ajili yakupata elimu kuhusu huduma za Kibanki zinazotolewa na Benki hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo.
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa Ecobank Tanzania mara baada kupata elimu kuhusu huduma za Kibanki zinazotolewa na Benki hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo.
No comments:
Post a Comment