Waziri
wa Maji Jumaa Aweso, (katikati mwenye shati la bluu) akiwa kwenye ziara
ya kukagua mradi wa Maji Mwakitolyo wilayani Shinyanga, wa tatu kushoto
ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko.
Na Marco Maduhu, Shinyanga
Waziri
wa Maji Jumaa Aweso, ametembelea ujenzi wa mradi wa maji Mwakitolyo
uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, na kutoa siku 10 mradi huo
uwe umekamilika na kutoa huduma ya maji kwa wananchi.
Aweso amefanya ziara hiyo Jumatatu Aprili 26,2021 , akiambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba.
Amesema
kati ya miradi ya maji 177 ambayo ni kero hapa nchini, mmoja wapo ni
mradi huo wa Mwakitolyo hivyo kuagiza hadi ifikapo Mei 5 mwaka huu ndani
ya siku 10 zijazo, uwe tayari umeshakamilika.
"Mradi
huu wa maji Mwakitolyo nina historia nao, ni kati ya miradi ya maji
kichefuchefu hapa chini, hivyo naagiza hadi ifikapo Mei 5 uwe tayari
umeshakamilika, sitaki kuzinguliwa na Rais, nadhani siku ile Bungeni
mlisikia Rais alivyosema, na kiu yake kubwa ni wananchi wapate maji,"
amesema Aweso.
"Pia
ma-Meneja Wakala wa maji vijijini Ruwasa, naagiza mfanye kazi kwa
kishirikiana na wakuu wa mikoa ,wilaya, na Madiwani, ili kuhakikisha
mnafanya kazi zenu kwa ufanisi na kuhudumia wananchi maji safi na
salama," ameongeza.
Katika
hatua nyingine Aweso amesema, Wakandarasi wasio na uwezo hawana nafasi
kupewa kazi za ujenzi wa miradi ya maji kwenye wizara hiyo, pamoja na
Wahandisi wa maji ambao ni wazembe watawajibishwa, huku akiahidi kutoa
Sh. milioni 100 kwa ajili ya kujenga Tenki lingine la maji lenye lita
Laki Tano kwenye mradi huo.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ameipongeza Serikali kwa
kutoa fedha kujenga mradi huo wa maji Mwakitolyo, na kuahidi kuusimamia
ili ukamilika kwa siku hizo 10 ambazo zimetolewa na kutoa huduma ya maji
safi na salma kwa wananchi.
Aidha
ameongeza kuwa, wao kama Serikali mkoani Shinyanga wapo vizuri kwenye
usimamizi wa ujenzi wa miradi ya maji, ambapo wiki ya madhimisho ya maji
walizindua miradi mingi ya maji ukiwamo wa Ihapa, Salawe, Mwamashele na
Mwawaza huku miradi mingine wataendelea kuizindua ukiwemo wa Masengwa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa
Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water
Supply and Sanitation Authority(KASHWASA) Mhandisi Joshua Mgeyekwa,
ambao ndiyo watekelezaji wa mradi huo wa maji Mwakitolyo kwa
kushirikiana na (RUWASA), alimhakikishia Waziri Aweso kuwa mradi huo
utakamilika ndani ya siku hizo 10, ambapo ujenzi wake ulianza mwaka
2020 na utagharimu Sh. bilioni 2.3.
Waziri
wa Maji Jumaa Aweso akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi
wa maji safi na salama Mwakitolyo wilayani Shinyanga.
Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye ziara ya
Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwenye ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa maji
Mwakitolyo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mbonekom akielezea mradi huo wa maji namna utakavyosaidia wananchi wa Mwakitolyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama
na Shinyanga (Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation
Authority(KASHWASA) ,Mhandisi Joshua Mgeyekwa (wa pili kushoto),
akielezea namna watakavyo kamilisha mradi huo wa maji Mwakitolyo.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiendelea kukagua ujenzi wa mradi wa maji Mwakitolyo.
Ukaguzi ukiendelea.
Mtambo ukiendelea na shughuli ya kufukia mabomba ya maji.
Waziri
wa Maji Jumaa Aweso (mwenye shati la bluu katikati) akiwa kwenye ziara
ya kukagua mradi wa Maji Mwakitolyo wilayani Shinyanga, wa tatu kushoto
ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
No comments:
Post a Comment