Na Amiri Kilagalila, Njombe
Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Mpainduzi (UWT) Wilaya ya Njombe,imeafanikiwa kupata mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Bi,Beatrice Malekela aliyepata kura 345 za wajumbe wa jumuiya hiyo katika uchaguzi uliofanyika mjini Njombe ili kupokea nafasi iliyoachwa wazi na mwenyekiti wa awali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa uchaguzi huo Hanafi Msabaha ambaye ni katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilya ya Njombe amesema uchaguzi huo mdogo umefanyika ikiwa umebaki mwaka mmoja kabla ya kuingia katika uchaguzi mkuu wa viongozi ndani ya Chama kwa lengo la kuziba nafasi inayoachwa wazi na Mwenyekiti wa awali Bi,Anjela Mwangeni ambaye ni diwani wa viti maalum halmashauri ya mji wa Njombe aliyeachia nafasi hiyo ili kubakiwa na nafasi ya udiwani kutokana na utaratibu wa Chama hicho.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi amewataja wagombea watatu waliokuwa katika nafasi hiyo akiwemo Rehema NgoziNgozi aliyepata kura 95,Julieth Kadodo kura 33 na mshindi wa nafasi hiyo Beatrice Malekela aliyeshinda kwa kura 345 huku akiwataka wanawake hao kushikamana kwani chaguzi zote za CCM wao ndio wanaotegemewa.
“Jumuiya ya akina mama ni jumuiya kilanja katika jumuiya za CCM kwa ushindi wa CCM tunategemea jumuiya ya wakina mama nchi nzima kwa kuwa mmekuwa waaminifu,mnachapa kazi”alisema Msabaha
Awali mwenyekiti aliyechia nafasi hiyo Bi,Anjela Mwangeni alitumia fursa hiyo kuwashukuru wajumbe hao kwa kumuamini na kumpa ridhaa ya kuwatumikia katika kipindi cha miaka 9 na kwamba wanapaswa kuendelea kumtumia katika nafasi yake ya udiwani pamoja na kumpa ushirikiano mwenyekiti mpya.
“Jumuiya ya wanawake inatakiwa isimame,ninaomba yaendelezwe yale tuliyokuwa tunaendelea nayo”alisema Anjela Mwangeni
Aidha mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo mwenyekiti mpya wa UWT wilaya ya Njombe Beatrice Malekela amesema atakuwa bega kwa bega na wanawake wote katika kuhakikisha jumuiya yao inasonga mbele.
“Nimekuwa
nikitenda kazi maeneo mengine lakini pia kwa fursa niliyo nayo nitahakikisha
vikundi vyote vinakuwa kimaendeleo,nitakuwa bega kwa bega na wanawake
kuhakikisha wanapewa mikopo kama inavyostahili”alisema Beatrice.
Beatrice
Malekela mwenyekiti mpya wa UWT wilaya ya Njombe akizungumza na wanawake wa UWT
mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi mdogo
uliofanyika katika ukumbi wa Turbo na kuahidi ushirikiano katika
majukumu ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment