HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 2, 2021

RAIS DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AMEMUAPISHA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR IKULU ZANZIBAR

 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Othman Masoud Othman kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. leo 2-3-2021.(Picha na Ikulu)
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mteule Mhe. Othman Masoud Othman akiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar akisubiri kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika leo 2-3-2021.Ikulu Zanzibar (Picha na Ikulu)
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe.Zuberi Ali Maulid na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji, wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masod Othman, iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapishwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mteule Mhe.Othman Masoud Othman, iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 2-3-2021.(Picha na Ikulu)
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mteule Mhe. Othman Masoud Othman akiwa amesimama wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapishwa iliofanyika leo 2-3-2021, katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAKUU wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar na Viongozi wa Dini wakifuatilia kuapishwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Mhe. Othman Masoud Othman, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akisaini hati ya kiapo baada ya kumalizika kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Hussein Ali Mwinyi, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha na pamoja na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliosimama nyuma na waliokaa kutoka (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad